THBUB:TUNATAMBUA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WAFANYAKAZI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 1, 2023

THBUB:TUNATAMBUA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA BORA KWA WAFANYAKAZI


Na Okuly Julius-Dodoma

TUME ya haki za binadam na utawala Bora(THBUB) imesema kuwa inatambua na kupongeza juhudi mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuinua maslahi na kuweka mazingira bora ya wafanyakazi Nchini.


Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe. Mohamed Khamis Hamad
alipokuwa akitoa Salamu wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani alisema kuwa hivi karibuni, THBUB imeshuhudia kupandishwa mishahara, posho za kujikimu na kupandishwa vyeo kwa watumishi wa umma nchini.


"Pamoja na jitihada hizo, THBUB imekuwa ikipokea na kushughulikia malalamiko kutoka kwa wafanyakazi yanayohusu maslahi yao kama vile kutopewa mkataba wa ajira, kutopandishwa madaraja, kutolipwa mishahara, kutopatiwa majibu ya rufaa zao na mamlaka za nidhamu, kupunjwa au kutolipwa posho mbalimbali ikiwemo posho ya kujikimu, posho ya likizo, posho ya kukaimu, posho ya kusafirisha mizigo, n.k,"alisema.


Aidha alisema kuwa Serikali na waajiri waendelee kusimamia utekelezaji wa Katiba, sheria za ajira na kuweka mazingira bora ya kazi ili kuhakikisha ajira zinazingatia heshima na utu wa mtu.


"Katika kuhakikisha usimamizi wa viwango vya ajira nchini, ni muhimu pia Serikali kupitia taasisi zinazohusika chini ya Wizara zinazohusika na Kazi, Ajira na Utumishi wa Umma Tanzania Bara na Zanzibar kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara,hususan katika sekta binafsi ili kuhakikisha haki za wafanyakazi kama zilivyobainishwa katika sheria zinazohusiana na masuala ya ajira zinazingatiwa ikiwa ni pamoja na malipo ya mishahara kwa wakati na yenye kuzingatia kiwango cha chini cha mishahara, usalama na afya mahali pa kazi, matibabu, malipo ya fidia inayotokana na kuumia kazini na michango ya hifadhi ya jamii,"alisema.


Kadhalika alisema kwa kuzingatia kuwa haki inaendana na wajibu, THBUB inawakumbusha wafanyakazi wote kutekeleza majukumu yao kwa juhudi na maarifa na kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia ajira zao. Aidha, wafanyakazi wajielekeze katika kuzingatia maadili na kutoa huduma zenye viwango kwa uadilifu

No comments:

Post a Comment