Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Mhe.Hamad Hassan Chande,akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Leo Mei 3,2023 Jijini Dodoma. |
Kamisaa wa Sensa Tanzania Bara na Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda,akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Leo Mei 3,2023 Jijini Dodoma. |
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa,akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Leo Mei 3,2023 Jijini Dodoma. |
Na Okuly Julius-Dodoma
Naibu Waziri, Wizara ya Fedha na Mipango Mhe.Hamad Hassan Chande amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kufanya kazi kwa weledi,kujituma na kwa umoja huku wakizingatia maadili ya utumishi wa Umma ili kufikia malengo katika kazi zao.
Mhe.Chande ameyasema hayo leo Mei 3,2023 Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Wafanyakazi wa Ofisi hiyo.
"Ili kufikia malengo na kutekeleza adhma ya serikali ni muhimu kujiandaa kufanya kazi kwa kujituma na kwa kuzingatia weledi na umoja nia ni kuhakikisha mnafikia malengo katika kazi zenu ikiwemo kuzitumia takwimu,"
"Serikali inatambua umuhimu wenu na ndio maana inapitia upya maslahi yenu ili muweze kufanya kazi kwa maslahi ya taifa na ikitokea fursa ya kwenda kuongeza ujuzi nenda kwa sababu ukiongeza maarifa naamini kuwa hata utendaji kazi utaongezeka na utakuwa na ufanisi mkubwa,"amesema Chande
Pia Mhe.Chande amesema Serikali itahakikisha kuwa itatumia matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa mafanikio makubwa ikiwemo kupanga na kupeleka miradi ya maendeleo kwa usawa kulingana na idadi ya watu wanaopatikana kwa eneo husika.
"Serikali haipo tayari kuona gharama kubwa zilizotumika kuandaa na kuendesha zoezi la Sensa ya watu na makazi lililofanyika 2022 zinapotea bure ni lazima Matokeo yale yatuletee faida chanya,"amesisitiza Chande
Naye Kamisaa wa Sensa Tanzania Bara Anne Makinda, amesisitiza kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kutumia maarifa waliyoyapata katika kuwaletea wananchi maendeleo kwani matokeo hayo ndio mlango wa serikali katika kufanya maendeleo
Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa ameeleza changamoto iliyopo kwa sasa ambapo amesema ni ongezeko la matumizi ya takwimu katika kufanya maendeleo, hivyo kuwaomba viongozi hasa wa kisiasa kuwa sehemu ya wanaotoa elimu juu ya umuhimu wa matokeo ya takwimu ili kuwaletea wananchi maendeleo
No comments:
Post a Comment