Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA, Prof. Mark Mwandosya ( kushoto) akisalimiana na Meneja Mradi wa UNDP, Aaron Cunningham baada ya kuwasili katika Ofisi za UNDP, Mlimwa C Dodoma Leo 30 Mei 2023. Kulia ni Kaimu Mkurugezi wa Umeme, EWURA, Mha. Victor Labaa na wa pili kushoto ni Mratibu wa Mradi wa Matumizi Bora ya Nishati, kutoka Wizara ya Nishati, Bw.Emilian Nyanda.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA, Prof. Mark Mwandosya akiweka chaja kwenye moja ya gari inayotumia umeme.
Mwenyekiti wa Bodi ( wa tatu kulia) Prof. Mark Mwandosya akitizama namna gari inayotumia umeme inavyochajiwa. UNDP wametengeneza vituo vya kuchaji magari ya umeme unatokana na nguvu za jua.
Moja ya kituo cha kuchaji magari yanayotumia umeme kilichopo katika Ofisi za UNDP Mlimwa C Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi EWURA, Prof. Mark Mwandosya akiingia kwenye gari inayotumia umeme katika Ofisi za UNDP Mlimwa C Dodoma. Anayetizama kulia, ni Mjumbe wa Bodi ya EWURA na Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati ya Bodi hiyo Bw.Harun Masebu.
Paneli za sola zinazotumika kuzalisha umeme unatokana na nguvu ya jua, Ofisi za UNDP Mlimwa C Dodoma
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi EWURA,Prof Mark Mwandosya, akiwa katika gari inayotumia umeme Leo 30 Mei 2023, eneo la Mlimwa C,UNDP, Dodoma
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi EWURA Prof Mark Mwandosya, akitama mfumo wa kuchaji magari kwa umeme unavyofanya kazi katika kituo cha kuchaji magari ya umeme, Ofisi ya UNDP, Mlimwa C Dodoma
Na.Mwandishi Wetu-DODOMA
Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Prof. Mark Mwandosya, leo 30 Mei 2023 ametembelea Mradi wa Utekelezaji Mpango wa Matumizi Bora ya Nishati katika Ofisi ya Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) jijini Dodoma ili kuona namna mradi huo unavyofanya kazi.
Meneja Mradi wa UNDP, Bw. Aaron Cunningham, amemweleza Prof. Mwandosya kwamba, mradi huo umelenga kuhakikisha upatikanaji wa uhakika na endelevu wa nishati ya kisasa kwa matumizi ya magari, viwanda na majumba makubwa.
Bw. Cunnighanm ameishukuru EWURA kwa ushirikiano na kueleza kwamba ina nafasi adhimu kwenye kuandaa na kusimamia kanuni za uendeshaji wa sekta ya umeme.
Prof. Mwandosya amepongeza jitihada hizo na kueleza kwamba, EWURA itaendelea kushirikiana na watoa huduma ili kuhakikisha matumizi bora ya nishati na ubora wa huduma zinazotolewa.
No comments:
Post a Comment