“SERIKALI KUJENGA VITUO MAALUM VYA UREKEBU” WAZIRI MHAGAMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 31, 2023

“SERIKALI KUJENGA VITUO MAALUM VYA UREKEBU” WAZIRI MHAGAMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa Taarifa kuhusu hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2022 kwa waandishi wa habari tarehe 30 Mei, 2023 Jijini Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2022 aliyoitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama alipokutana nao Mei 30, 2023.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2022 aliyoitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama alipokutana nao Mei 30, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati), Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini Bw. Aretas Lyimo (kushoto) pamoja na Kamishna wa Kinga na Tiba kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Dkt. Peter Mfisi (kulia) wakionesha nakala za kitabu chenye Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2022 wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari Jijini Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na; Mwandishi Wetu – Dodoma


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, amesema Serikali imejenga vituo maalum vya urekebu na ufundi stadi ili kuwasadia vijana na wale wote wanaoathirika baada ya kutumia dawa za kulevya.


Ameyasema hayo mapema Mei 30 2023, Bungeni Dodoma wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2022 ambapo amessema kwa mujibu wa utafiti unaonyesha uwepo wa kiwango kikubwa cha uzalishwaji na ulimaji wa bangi.


Waziri Mhagama alisema, kwa mwaka ujao wa fedha 2023/2024 Serikali imetenga bajeti ya shilingi Bilioni nane nukta saba (Bilioni 8.7) zitakazotumika kujenga vituo vya urekebu na ufundi stadi, vitakavyosaidia kubadilisha tabia za vijana wanaotumia dawa za kulevya,


“Vituo hivyo vitakuwa na kazi kubwa ya kuwaondoa kwenye matumizi ya dawa na kuwapa shunguli nyingine watakazotakiwa kuzifanya zitakazotokana na shughuli za ujuzi, ambazo watafundishwa kwenye vitu hivyo.” Alifafanua.


Aliendelea kusema kuwa, kupitia Wizara ya Kilimo, Serikali itafanya utafiti, ili maeneo yanayolima bangi kibiashara kama vile Kisimiri Juu mkoani Arusha, kusaidiwa kulima mazao mbadala na juhudi za Serikali za kukomesha kilimo hicho zinaweza kuwasaidia kutoka kwenye biashara hiyo haramu kwa makusudi ya kuongeza kipato, na kuwafanya vijana na watumiaji kuwa salama.


“Kwa Jiji la Dodoma pekee tunategemea kutumia kiasi cha shilingi Bilioni mbili, kujenga kituo hicho katika Eneo la Itega.” Alisema.


Awali akiongea katika mkutano huo na waandishi wa habari aliitaja baadhi ya mikoa inayoongoza kwa kulima bangi nchini kuwa ni pamoja na Arusha, Manyara, Mara na Njombe,na kuitaja baadhi ya Mikoa itakayojengwa vituo hivyo kuwa ni pamoja na Shinyanga, Kilimanjaro, Mwanza na Arusha.

No comments:

Post a Comment