TAASISI ZINAZOCHOCHEA MAPENZI YA JINSIA MOJA KUCHUNGUZWA -MHE.MASAUNI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 29, 2023

TAASISI ZINAZOCHOCHEA MAPENZI YA JINSIA MOJA KUCHUNGUZWA -MHE.MASAUNI


Na,Mwandishi wetu -Dodoma.


Katika kudhibiti na kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili kwenye Jumuiya za Kidini na zisizo za Kidini, Ofisi ya Msajili wa Jumuiya imesitisha shughuli za Jumuiya ya kidini iitwayo Spirit Word Ministry kwa sababu ya kutoa mahubiri na mafundisho yenye mwelekeo wa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya Jinsia Moja na kufifisha jitihada za mapambano ya vitendo vya ushoga nchini.


Hayo yamebainishwa na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe. Hamad Masauni Leo Mei 29, 2023 bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 ambapo amesema Jumuiya hiyo ya kidini iitwayo Spirit Word Ministry iliyopo eneo la Stakishari Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam imefutiwa usajili wake.


“Jumuiya hiyo imefutiwa usajili kwa sababu ya kutoa mahubiri na mafundisho yenye mwelekeo wa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na kutoa ujumbe wenye kufifisha jitihada za kupambana na vitendo vya ushoga nchini” amesema  Masauni.


Vilevile ameweka bayana taarifa kukusanywa zinazohusu idadi ya vituo vya kulea watoto na shule zinazotoa mafundisho ya dini kwa watoto wadogo huku Lengo likiwa ni kutambua idadi ya vituo au shule za bweni zinazotoa mafunzo yenye mwelekeo unaokinzana na maadili ya nchi yetu ikiwemo vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.


Jitihada za serikali nazo si haba katika kukabiliana na vitendo vinavyokiuka Mila na desturi za nchi ikiwa ni pamoja na elimu kutolewa kwa Viongozi wa Jumuiya za Kidini.


“Kazi ya kuboresha vigezo vya usajili inaendelea kwa lengo la kuhakikisha kuwa Jumuiya zinazosajiliwa ni zile zenye kuleta tija na zisizokinzana na mila, desturi na utamaduni wa Kitanzania” amesema Masauni


Hata hivyo serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu mienendo ya jumuiya zote na kuchukua hatua kali kwa watu au jumuiya zitakazo hamasisha vitendo vya ukiukwaji wa maadili.

No comments:

Post a Comment