Katika kuhakikisha huduma ya ukaguzi wa maeneo yanayotumia vyanzo vya mionzi pamoja na utoaji wa vibali kwa mionzi Serikali kupitia Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania inaendelea na ujenzi wa maabara pamoja na ofisi Zanzibar ambapo ujenzi umefikia asilimia 83%.
Akizungumza kando ya ujenzi unaoendelea Mkuu wa Ofisi ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania upande wa Zanzibar Bwn. ALI OTHMAN MASOOD amesema anaishukuru Serikali inayoongozwa na Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN kwa uamuzi wa kujenga ofisi hiyo ambayo itakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo upande wa Zanzibar.
MASOOD amesisitiza kwamba utoaji wa vibali vya mionzi kwa wanaostahili pamoja na ukaguzi wa watumiaji wa vyanzo vya mionzi kutaimarishwa na ofisi pamoja na maabara zinazojengwa hivi sasa.
Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania DKT. JUMA SALUM MBWANA amesema kukamilika kwa ujenzi huo ambapo kwa sasa umefikia asilimia 83 ili kukamilika kwake kutasaidia sana kupatikana kwa ajira kwa vijana waliosomea fani mbalimbali.
Sambamba na hayo Dkt. JUMA amemshukuru Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. HUSSEN ALI MWINYI kwa kuwezesha ujenzi wa barabara ya lami kufika ofisini hapo pamoja na kuridhia kuiongezea TAEC eneo kwa ajili ya upanuzi wa majengo mengine ya kimkakati yatakayojengwa eneo hilo la Dunga Zuze.
No comments:
Post a Comment