Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wametakiwa kuachana na vitendo vya Rushwa vya kutaka kufaulishwa Katika masomo yao na wahakikishe wanakuwa mstari wa mbele kupinga na kuzuia vitendo vya Rushwa
Hayo yamesemwa na Rasi wa Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati Prof. Said Vuai wakati akifungua Warsha ya utoaji wa Elimu juu ya kupiga vita vitendo vya Rushwa pamoja na Elimu ya jinsia.
Warsha hiyo imewajumuisha wanafunzi pamoja na wahadhiri wa Chuo hicho kilichofanyika Jijini Dodoma huku akiwataka walimu waachane na vitendo vya Rushwa vya kuwarubuni wanafunzi kwa kuwapa msaada wa kuwafaulisha.
Amesema hakuna maendeleo bila ya haki na haki haiwezi kupatikana kama kuna Rushwa hivyo kama kijana ametumia njia ya kufaulu kwa njia ya Rushwa basi hata Katika maeneo ya kazi atakayoenda yatakuwa na changamoto na kusababisha Rushwa.
Kwa upande wake Mchunguzi kiongozi Taasisi ya Kuzua na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma Faustine Malecha amesema kuwa zipo tabia ambazo zinapelekea Rushwa Moja wapo ni kuiga vitu ambavyo sio desturi ya watu wa Kitanzania vinapelekea vijana hawa kujikita katika Rushwa huku akifafanua aina za Rushwa na kusisitiza vijana waache kutumia Rushwa ya ngono kwa kuhisi watafanikisha maisha kwa haraka.
Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kina mama na uzazi Dr. Gabriel Kitunusa amesema kuwa wanafunzi wengi wanapata Elimu zisizo rasmi huko mitaani kuhusiana na mambo ya jinsia na mambo ya uzazi na kupelekea kupata changamoto za kutoa mimba na kusababisha Vifo.
Pia amesema changamoto kubwa ambao wanafunzi hawa wanakutana nazo ni kupata mimba zisizotarajiwa na wengine kupata maambukizi ya VVU pamoja na Magonjwa ya zinaa hivyo amewataka waachane na Elimu ya mitaani na waachane na mienendo mibovu ya kimaadili.
Ikumbukwe kuwa Ndaki ya Sayansi Asilia ya Hisabati inajukumu la kufundisha , kufanya utafiti kutoa huduma kwa jamii kupitia utaalamu wa utafiti pamoja na malengo mengine yanayohusiana na Rushwa na maswala ya Afya.
No comments:
Post a Comment