KIKWETE ATAO RAI KWA TAKUKURU KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 15, 2026

KIKWETE ATAO RAI KWA TAKUKURU KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Viongozi na Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara yake ya kikazi iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akizungumza maneno ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete kuzungumza na Viongozi na Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara ya kikazi iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila wakati Waziri huyo alipotembelea Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakati wa ziara yake ya kikazi iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila akielezea utekelezaji wa majukumu ya ofisi hiyo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo iliyofanyika jijini Dodoma.

Na. Mwandishi Wetu-Dodoma


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ametoa rai kwa Menejimenti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 hususani katika eneo la utawala bora kuweka mikakati ya pamoja ya kuzuia na kupambana na rushwa na kuhakikisha watumishi wao wanafanya kazi kwa kuzingatia uwazi, usawa na uwajibikaji.

Mhe. Kikwete ametoa rai hiyo Januari 15, 2026 jijini Dodoma wakati alipotembelea Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa lengo la kuzungumza na watumishi hao na kujitambulisha.

“Mimi na msaidizi wangu Mhe. Regina Qwaray tunaipongeza Menejimenti na Watumishi kwa kuteleza majukumu yenu kwa weledi na ufanisi, pia niwahakikishie kuwa sisi tuko tayari kutoa ushirikiano wa dhati wakati wote ili taasisi yetu iendelee kuaminiwa” alisema Mhe. Ridhiwani.

Pia, ameitaka TAKUKURU kutangaza na kusema mafanikio inayoyapata katika utendaji kazi wao na kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari hususani mitandao ya kijamii ambayo kwa sasa ni chombo muhumu cha mawasiliano katika jamii.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray aliongeza kuwa pamoja na kufika kujitambulisha, pia wamekwenda kuwakumbusha watumishi hao wajibu wao ili kuweka mshikamano na umoja katika usimamizi wa miradi ya maendeleo nchini.

“Tumekuja kujitambulisha ili tupate kufahamiana, hivyo ninaomba tuongeze ari ya kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufanikisha maono ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo wananchi” alisema Mhe. Qwaray.

Naye, Bi. Enedy Munthali kwa niaba ya Katibu Mkuu - Ofisi ya Rais Ikulu amesema kuwa Ofisi yake iko tayari kuendelea kuhakikisha TAKUKURU inapata rasilimaliwatu na fedha kwa mujibu wa bajeti yao ili kukamilisha majukumu na miradi kwa wakati.

Pia, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila amewashukuru mawaziri hao kwa kuitembelea taasisi hiyo na ameahidi kwa niaba ya Menejimenti na Watumishi wa ofisi hiyo kutoa ushirikiano kwa viongozi hao ili kutekeleza majukumu kwa ufanisi.

Vile vile, TAKUKURU inaendelea kufanya utafiti ili kubaini mianya ya rushwa na kuzuia na kuhakiksha wananchi wanapata huduma bora kama Serikali ya inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ilivyokusudia.

Awali, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi. Neema Mwakalyelye alimuomba Mhe. Kikwete kufikisha salamu za shukurani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

No comments:

Post a Comment