Wanamichezo wa JWTZ Waibuka Kidedea Mashindano ya Majeshi Duniani - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 24, 2023

Wanamichezo wa JWTZ Waibuka Kidedea Mashindano ya Majeshi Duniani


Na Immaculate Makilika – MAELEZO

 

Serikali imesema kuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) imeshiriki katika michezo mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo mashindano ya Dunia ya Michezo ya Majeshi yaliyofanyika Ujerumani, mwezi Julai 2022, Michezo ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika Birmingham nchini Uingereza mwezi Agosti 2022, Mashindano ya Ngumi ya Ukanda wa Afrika yaliyofanyika nchini mwezi Agosti 2022, East African Championship yaliyofanyika Burundi mwezi Septemba 2022.

 

Aidha, mashindano mengine ni Mashindano ya Gofu yaliyofanyika Lilongwe nchini Malawi mwezi Novemba 2022, Michezo ya Majeshi (BAMMATA) iliyofanyika mkoani Mtwara mwezi Februari 2023, Mashindano ya Riadha yaliyofanyika nchini Japan 17 (Osaka Marathon) na China (Yangzhou Jianzhen International Half Marathon) mwezi Februari na Aprili 2023 mtawalia.

No comments:

Post a Comment