WAZIRI MHAGAMA AWATAKA WAKANDARASI UJENZI WA MJI WA SERIKALI MTUMBA KUONGEZA KASI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, May 7, 2023

WAZIRI MHAGAMA AWATAKA WAKANDARASI UJENZI WA MJI WA SERIKALI MTUMBA KUONGEZA KASI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na timu aliyoambatana nayo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa majengo ya ofisi za Serikali Mtumba Dodoma, ziara ilifanyika tarehe 6 Mei, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na timu aliyoongozana nayo wakikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii Mjumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelekezo kwa wakandarasi wanaosimamia ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa majengo ya ofisi za Serikali Mtumba Dodoma, ziara ilifanyika tarehe 6 Mei, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Shirika la Nyumba la Taifa NHC Mhandisi Aikani Mlekeo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi Awamu ya Pili katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.
Mhandisi kutoka NHC, Grace Musita akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama muonekano wa ramani ya jengo la Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mtumba Dodoma.
Mratibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Serikali Kuhamia Dodoma na Msimamizi wa ujenzi wa Mji wa Serikali Bw. Meshack Bandawe akifafanua jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ziara yake Mji wa Serikali Mtumba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akioneshwa majengo ya Ofisi ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Meja Salum Jambo ambaye ni msimamizi wa mkandarasi wa mradi huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa eneo la Mashujaa katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Mkandarasi kutoka Chuo Kikuu cha Adhi, Sauden Anania akielezea maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama leo Mei 6, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama mwenye koti la pink) pamoja na timu aliyoongozana nayo wakitembelea jengo la ofisi yake Mtumba Dodoma, wakati wa ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akikagua ujenzi unaoendelea wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na, Mwandishi Wetu – Dodoma


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama, amewataka wakandarasi wanaondelea ya shughuli ya ujenzi wa majengo ya Mji wa Serikali Mtumba Dodoma kuongeza kasi, na kufanya vikao vya mara kwa mara ili kuweza kutatua changamoto za ujenzi wanazokutana nazo.


Waziri Mhagama ameyasema hayo leo Mei 6, 2023 alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa baadhi ya majengo hayo na kuwaasa wakandarasi hao kujenga majengo yanayoendana na thamani ya fedha zilizopangwa na kuhepuka ucheleweshwaji ili kufikia malengo ya Serikali.


“Fanyeni kazi kwa pamoja na kuhakikisha mnaongeza kasi ya ujenzi, muwe na site meetings, tatueni changamoto kwa wakati, thamani ya fedha ilingane na mradi na thamani ya mradi iendane na fedha, hatuhitaji kuwa na delays yoyote katika ujenzi wa mradi huu,”alisema Mhe. Mhagma


Alipokuwa katika Jengo la Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, aliwaasa Wakandarasi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kutumia fursa ya ujenzi wa Mji wa Serikali kwa kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kuuza ujuzi kwa wageni watakaotembelea mji huo wa Serikali mbeleni na kuwawezesha kuteka soko la Nchi za Afrika Mashariki na nchi za kusini mwa Afrika.


Kwa Upande wake Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara hiyo kutoka Shirika la Nyumba la Taifa NHC Mhandisi Aikani Mlekeo Alisema “ Tunaishukuru Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu chini ya Usimamizi wa mratibu wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Bw. Mesharck Bandawe, kwa kutupa Mwongozo mzuri katika usimamizi wa Ujenzi wa Mradi huu.”


Ziara hiyo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, ilihusisha kutembelea na kukagua baadhi ya ujenzi wa majengo ya Serikali ikiwa ni pamoja Eneo la ujenzi wa Mradi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu na Eneo linalojengwa Uwanja wa Mashujaa.

No comments:

Post a Comment