Akizungumza katika kikao kazi hicho, Waziri wa Elimu Mhe. Prof. Adolf Mkenda amesema Wizara itaendelea kushirikiana na wadau hao katika kuhakikisha mageuzi ya elimu yanayofanyika yanafanikiwa.
"Mageuzi haya tunayofanya yanahitaji rasilimali katika kuyafanikisha, tuendelee kushirikiana ili yaweza kufanikiwa nasi tutaendelea kuwashirikisha katika kila hatua”,amesema Prof. Mkenda
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Carolyne Nombo amewashukuru wadau hao kwa namna wanavyoendelea kufadhili miradi ya elimu yenye lengo la kuendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo ya Elimu ambae pia ni Mkuu wa Sekta ya Elimu UNESCO Faith Shayo ameipongeza Serikali kwa mageuzi makubwa yanayofanyika kwenye elimu huku akiishukuru Wizara kwa kuwashirikia katika hatua mbalimbali kuelekea mageuzi hayo.
No comments:
Post a Comment