Na Okuly Julius-Dodoma
Agizo hilo, limetolewa Juni 1,2023 Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi mara baada ya kuzindua bodi hiyo na mradi wa Majisafi Ntyuka Chimalaa wenye thamani ya sh. milioni 471.8.
Mahundi ameisisitiza bodi hiyo kushirikiana na Watumishi kuweka mikakati ya kuendelea kupunguza kiasi hicho cha upotevu wa maji ili kufikia chini ya asilimia hiyo kwa miaka ijayo.
Pia, ameiagiza bodi hiyo kushirikiana na watumishi kuweka mikakati ya kuendelea kuongeza makusanyo ili Mamlaka iweze kuboresha utoaji wa huduma huku akiipongeza Bodi iliyopita kwa kuongeza makusanyo kutoka Sh. Bilioni 1.7 hadi bilioni 2.2 kwa mwezi.
Aidha, ameiagiza bodi hiyo kuendelea kuwahudumia ipasavyo wakazi wa Dodoma huku ikitekeleza miradi ya muda mfupi ya kupunguza changamoto ya ukosefu wa maji wakati serikali ikitekeleza miradi mikubwa.
Vilevile, ameiagiza bodi hiyo kushirikiana na Menejimenti ya DUWASA kuendelea kusimamia ipasavyo miradi yote ya maji pamoja na kuhakikisha uwepo wa thamani ya fedha katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Mbali na hilo ameitaka kuendelea kuangalia maslahi ya Watumishi wa DUWASA ili kuwaongezea kasi ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Awali akizungumza mara baada ya kuzindua mradi wa maji, Mahundi ameeleza kuwa dhamira ya Rais ya kumtua mama ndoo kichwani inaendeea kutekelezwa kwa vitendo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameshauri Dodoma kupewa mpango mkakati wa kipekee wa kutatua changamoto ya maji ili kuendana na uwepo wa makao makuu ya nchi.
Amesema Mkoa wa Dodoma kuna taasisi nyingi ambazo wanafanya nazo kazi huku akiitaja DUWASA kama Mamlaka inayofanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi, Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph amesema mradi huo unanufaisha wakazi wapatao 4,441 ambapo kati ya hao 1,931 wanaishi katika maeneo ya Ntyuka mtaa wa Chimalaa katika awamu ya kwanza, na awamu ya pili itanufaisha wakazi wapatao 2,510 katika mtaa wa Nyerere.
Amefafanua kuwa mradi huo ulitekelezwa na kukamilika kwa muda wa miezi sita huku lengo likiwa ni kuboresha hali ya upatikanaji maji kutoka asilimia 0 mpaka 95.
Mwenyekiti wa Bodi aliyemaliza muda wake , Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM), Profesa Faustine Bee amesema katika kipindi cha uongozi wao wamepata mafanikio mbalimbali ikiwemo kuongeza urefu wa mtandao wa mabomba ya kukusanya majitaka.
Naye, Mwenyekiti mpya wa bodi, Balozi Mstaafu Job Masima amemshukuru Waziri wa Maji kwa imani aliyomuonesha yeye na bodi na kuamua kumteua huku akieleza watatekeleza kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa na kuenzi yaliyoachwa na viongozi waliopita.
No comments:
Post a Comment