DKT. MSONDE ASISITIZA UADILIFU WAKATI WA MAPOKEZI YA NAIBU KATIBU MKUU MATIVILA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 20, 2023

DKT. MSONDE ASISITIZA UADILIFU WAKATI WA MAPOKEZI YA NAIBU KATIBU MKUU MATIVILA


 James Mwanamyoto ,OR-TAMISEMI 


Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Charles Msonde amewataka watumishi wa ofisi yake kuwa waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kutekeleza azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwa na utumishi wa umma wenye uadilifu na tija katika maendeleo ya taifa. 


Dkt. Msonde ametoa wito huo leo kwa watumishi wa TAMISEMI mara baada ya kumpokea Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhandisi Rogatus Mativila alieapishwa tarehe 16, Juni 2023 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma.


 Dkt. Msonda amesema, watumishi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI wanapaswa kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa kwani wanatekeleza majukumu yao kwa niaba ya mwenye dhamana ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. 


“Dhamana tuliyopewa ya kuitumikia ofisi hii inatulazimu kuwa mstali wa mbele katika kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya kiutumishi iliyopo, hivyo tunapaswa kuhakikisha tunafanya kazi kwa uadilifu ili tusimuangushe Mheshimiwa Rais,” Dkt. Msonde amesisitiza. 


Naye, Naibu Katibu Mkuu (Afya) Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Charles Mahera amemshukuru Mhe. Rais kwa kumteua Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila ili kuongeza nguvu ya kiutendaji katika Ofisi ya Rais-TAMISEMI na kuongeza kuwa, ni wajibu wa menejimenti kuhakikisha inafanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo. 


Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhandisi Rogatus Mativila ameiomba Menejimenti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kumpa ushirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu. 


Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Menejimenti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. John Cheyo amesema Menejimenti itatoa ushiriano wa dhati kwa Naibu Katibu Mkuu (Miundombinu) Mhandisi Rogatus Mativila ili aweze kutimiza wajibu wake ipasavyo.

No comments:

Post a Comment