MHE.NDEJEMBI AWATAKA NEMC KUCHUKUA HATUA KALI KWA WATIRIRISHA MAJI TAKA KWENYE MITARO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 3, 2023

MHE.NDEJEMBI AWATAKA NEMC KUCHUKUA HATUA KALI KWA WATIRIRISHA MAJI TAKA KWENYE MITARO


Na Okuly Julius-Dodoma

NAIBU waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Deogratius Ndejembi, ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote wanao tiririsha maji taka kwenye mitaro iliyojengwa maalum Kwa kupitisha maji ya mvua.


Ndejembi, ameyasema hayo leo Juni 3,2023 Jijini Dodoma, alipokuwa akizungumza na wakazi wa jiji la Dodoma mara baada ya kufanya usafi katika eneo la Mji mpya ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira duniani juni 5, mwaka huu.


Amesema, wakati akishiriki kufanya usafi katika mitaa ya barabara ya saba ya nane pamoja na ya tisa amebaini kuwa mitaro mingi ambayo imejengwa maalum kwa ajili ya kupitisha maji ya mvua wakati wa masika watu wanaitumia vibaya kwa kutiririsha maji taka.


“Niwagize NEMC, kufanya ukaguzi wa uchavuzi wa mazingira katika jijini la Dodoma hasa kwa watu hawa ambao wamekuwa wakitiririsha maji taka kwenye mitaro hii iliyojegwa na kwa yeyote atake bainia achukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine”amesema Ndejembi



Aidha, amewataka wakazi wa jiji la Dodoma kuendelea kufanya usafi kila wakati badala ya kuendelea kusubiri hadi siku za maadhimisho kama hayo.


“Usafi lazima uwe utamaduni wetu lakini leo nimeona pia watu wanatupa taka ngumu kwenye mitaro hali ambayo inasababisha kuziba hivyo basi taka ngumu zote zinapaswa kuhifadhiwa na kupakiwa kwenye magari ya taka kwenda dampo”amesema Ndejembi



Kadhalika amewataka viongozi wa mitaa, vitongoji,vijiji pamoja na kata kuhamasisha wananchi kushiriki kufanya usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kuendelea kuhifadhi mazingira.


“Niagize pia halmashauri zote nchini kila wanapopima viwanja wahakikishe kuwa wanapanda miti ili kufanya maeneo yote kuwa ya kijani lakini pia maeneo mengi ya wazi ambayo hivi sasa ni vumbi tupu yapandwe miti kama ilivyokuwa hapo zamani wakati tunayo Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), ambao walikuwa wana utaratibu wa kupanda miti katika maeneo ya mji na kuitunza”amesema


Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule, amesema wiki hii watanza utaratibu wa kukagua maeneo mbalimbali ya mji na watakapo baini watu kufanya uchafuzi wa mazingira hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bahi Godwin Gondwe, amesema wameanza kutekeleza maagizo ya serikali ya kuwa na kitalu cha miti na kwa kuanzia wametenga Sh. milioni 20 kwa ajili ya kustawisha miche ya miti na kuipanda katika maeneo mbalimbali.


Kilele cha maadhimisho ya wiki ya mazingira Kitaifa itanyika Juni 5,2023 ,Mgeni Rasmi akitarakiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango na yatafanyika Jijini Dodoma eneo la Soko la Machinga.

No comments:

Post a Comment