WAZIRI AWESO AWATAKA WATUMISHI WA SEKTA YA MAJI KUTUMIKIA KIKAMILIFU NAFASI WALIZONAZO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 27, 2023

WAZIRI AWESO AWATAKA WATUMISHI WA SEKTA YA MAJI KUTUMIKIA KIKAMILIFU NAFASI WALIZONAZO


Na Okuly Julius Dodoma

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewataka watumishi,Taasisi na Mamlaka zilizo Chini ya Wizara hiyo kuhakikisha wanatimiza majukumu yao Kwa Kila mmoja Kwa nafasi yake.


Mhe.Aweso ametoa kauli hiyo Leo Juni 27,2023 Jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye Hafla ya Uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Maji na Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).




Ambapo Mhe Aweso amesema kumekuwa na uwepo wa baadhi ya watendaji wasiotimiza majukumu yao jambo ambalo linakwamisha Wananchi kupata huduma ya maji katika baadhi ya maeneo.


"Kuna baadhi ya RM ambao hawajui hata miradi inaendeleaje unakuta Mradi wa bilioni 6 yaani Meneja wa Mkoa hata hajui umefikia wapi na ukimuuliza hana anachojua sasa katika Wizara hii ambayo maji hayana Mbadala hatutaki watu wa namna hiyo,"



Na kuongeza kuwa" tumemaliza kazi ya Bajeti kinachofuata sasa ni kwenda kufanya tathmini ya utendaji nitapita Kila Ofisi kuona utendaji wake na Mtu ukifanya kazi inaonekana hivyo tutawapima Kwa kazi na matokeo yake nawakumbusha tu maji hayana Mbadala na Mbadala wake ni wananchi wapate huduma ya maji,"amesema Aweso



Pia ameitaka Bodi Mpya ya Mfuko wa taifa wa Maji kutafuta vyanzo vingine vya mapato wasitegemee tu Kodi ya Mafuta ni vyema wakatafuta washirika wa kusaidia katika utekelezaji wa miradi.



Amesema Mfuko wa Maji ni kichochoe kikubwa Cha ukuaji wa Sekta ya Maji hivyo miradi inayotekelezwa isimamiwe ili ikikamilika iwe chanzo Cha mapato na kuwezesha Ujenzi wa Miradi mingine.


'sioni haja ya Mradi kusuasua Kwa kisingizio kuwa hakuna pesa na sioni haja ya mkandarasa ambaye tayari ameshawasilisha Certificate yake kucheleweshewa MALIPO yake walipeni watu pesa muwadai kazi,"amesema Aweso.



Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba amesema kwa sasa Wizara hiyo imeamua kuachana na utaratibu wa kuchimba visima vidogovidogo Kwa Kila Kijiji badala yake wanachimba kisima kikubwa na kusambaza maji katika vijiji vingi ili kupunguza gharama.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amesema kuwa Dodoma bado hakuna maji ya uhakika hivyo kaiomba Wizara ya Maji kufanya Dodoma kuwa ni eneo Maalum la kushughulikiwa kwani ni Makao Makuu ya nchi hivyo ongezeko la watu wanaohamia ni kubwa.


Pia amebainisha kuwa kutokuwepo Kwa maji ya uhakika imekuwa chanzo Cha kuwapoteza wawekezaji ambao wanatamani kuwekeza Jijini Dodoma.


"Kutokuwepo Kwa maji ya uhakika inaupotezea Mkoa wa Dodoma sifa Kwa wawekezaji maana wanapokuja jambo la kwanza kutuliza ni maji na wakigundua kuwa Kuna changamoto ya maji hawarudi tena hivyo Dodoma kama Makao Makuu itengewe fungu maalumu kuhakikisha changamoto ya maji inatatuliwa ili wawekezaji wavutiwe kuwekeza hapa," Senyamule




Kaimu Mkurugenzi Mkuu RUWASA  Bwai Biseko amesema lengo la Serikali la kuwapatia wananchi washio vijijini huduma ya majisafi na salama kwa wastani wa zaidi ya asilimia 85 ifikapo mwaka 2025 na asilimia 100 ifikapo mwaka 2030 litatimia.


Pia amezungumzia mafanikio ya usimamizi wa Bodi kwa Menejimenti ya RUWASA kuwa umewezesha kujenga miradi na ongezeko la upatikanaji wa huduma ya Maji kwa kiwango cha kutia matumaini katika maeneo ya vijijini



"RUWASA ilmetekeleza ujenzi wa miradi na kufanya ongezeko la upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wanaoishi vijijini kutoka asilimia 64.8 mwaka 2019 hadi kufikia asilimia 77 mwezi Disemba 2023,"



Na kuongeza"jumla ya miradi 5,715 ya ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji ilipangwa kutekelezwa kwa kipindi cha kuanzia Julai 2019 hadi Juni 2023 ikijumuisha Miradi 174 ya Programu COVID 19 na miradi 632 iliyopokelewa kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa wakati wa uanzishwaji wa RUWASA," amesema Biseko



Amebainisha kuwa katika kipindi hicho, maeneo 2,252 ya uchimbaji wa visima na ujenzi wa mabwawa 99 yalipangwa kutekelezwa, na usanifu wa miradi 1893. Hadi kufikia Desemba 2022, jumla ya miradi 2,273 ya miundombinu ilikuwa imejengwa na kukamilika kupitia fedha za ndani na wadau wa Maendeleo. Miradi hiyo inanufaisha wanachi 11,641,230 katika vijiji 4,809. Ka tika kipindi hicho ujenzi wa mabwawa saba ulikamilika na jumla ya visima 947 vilichimbwa.


No comments:

Post a Comment