Missenyi-Kagera
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso akiwa wilayani Missenyi Mkoani Kagera amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Eng.Nadhifa Kemikimba kusimamia na kuhakikisha maeneo yote yalio pembezo mwa ziwa Victoria na Mto Kagera yanapata maji ya uhakika.
Waziri Aweso amesisitiza kuwa muelekeo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ni matumizi ya Rasilimali toshelevu katika kuhakikisha watanzania wanafikiwa na huduma ya Maji.
Aidha, waziri Aweso amezindua mradi wa maji Katolerwa-lshozi leo wenye Gharama ya 823,642,795.19. Mradi unahudumia wananchi 7278. Vijiji vinavyohudumiwa ni luhano, katano, katolerwa na nyarugongo.
No comments:
Post a Comment