Bonde la mto Songwe kubadili maisha ya wananchi, Tanzania na Malawi - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 13, 2023

Bonde la mto Songwe kubadili maisha ya wananchi, Tanzania na Malawi


Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amehimiza nguvu zaidi katika kuleta maendeleo ya bonde la mto Songwe yaliyojikita katika kuinuia Maisha ya wananchi wa Tanzania na Malawi


Mhe. Aweso ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Mawaziri wa Kamisheni ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe (SONGWECOM) amesema hayo akifungua mkutano wa pili wa baraza hilo uliofanyika jijini Dar es salaam.


“Serikali ya Tanzania na Malawi, zinaweka nguvu kushirikiana katika katika kuendeleza bonde hili ina tusipoteze nguvu ambazo zimeshatumika na kutufikisha hapa tulipo” Mhe. Aweso amewaambia wajumbe wa mkutano huo wakiwamo viongozi wanaotoka Tanzania na Malawi.


Amesema majadiliano rasmi kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Malawi kwa ajili ya ushirikiano katika bonde hilo na kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa kudumuwa changamoto mbalimbali ikiwamo mafuriko yalianza mwaka 1976. 


Naye Waziri wa Maji wa Malawi Mh. Abida Sidik akiongea katika mkutano huo amesema bonde hilo litaendelezwa na kubadili maisha ya wananchi nan chi yake imejipanga katika kufanikisha miradi itakayobuniwa na wataalamu kutoka pande mbili za nchi nufaika, Tanzania na Malawi.


Kijiografia, mto Songwe ni sehemu ya Bonde la Ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania. Mto huu unaanzia katika milima iliyoko Wilayani Mbozi na kumwaga maji yake katika Ziwa Nyasa. Aidha Mto Songwe unaunda sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Malawi na una urefu wa kilometa 200. 


Bonde la Mto Songwe lipo kusini magharibi mwa Tanzania na kaskazini mwa nchi ya Malawi na lina ukubwa wa kilometa za mraba 4,243


Pamoja na mapendekezo ya ujenzi wa Mabwawa, usanifu wa kina (detailed design and investment preparation) imeandaliwa miradi 26 yenye thamani ya Dola za Marekani millioni 829 itakayotekelezwa kupitia Programu ya Kuendeleza Bonde la Mto Songwe. 


Programu hiyo inashirikisha sekta mbalimbali zikiwemo Maji, Nishati, Umwagiliaji, Ardhi, Kilimo, Hali ya Hewa, Mazingira, Serikali za Mitaa, Uwekezaji, pamoja na Sekta ya Viwanda na Biashara.

No comments:

Post a Comment