Na Mwandishi wetu -Dodoma
Mstaafu wa Mahakama mkoani hapa na mmiliki wa Mgahawa wa Chapatichapati jijini hapa, Sharifu Mussa Kasmiri alibainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa mgahawa huo.
Alisema kutokana wastaafu wengi nchini kuwekeza fedha zao kwenye miradi ambayo hawana uzoefu nayo mara baada ya kustaafu imekuwa ndiyo chanzo kikubwa cha vifo vyao.
“Wastaafu wengi miradi ambayo wanawekeza fedha zao za mafao ni ile ambayo hawana uelewa nayo ndiyo maana unakuta wengi wao wanakufa kutokana na presha kutokana na miradi hiyo kufa na wao kufilisika”alisema
Alisema ili kuondokana na tatizo hilo watumishi wa umma wanapaswa kuanzisha miradi yao kabla ya kustaafu ili wawe na uzoefu nayo na kujenga maiasha yao ya baadaye.
“Lazima watumishi wa umma kuwa na miradi ambayo itakusadia mara baada ya kustaafu ambayo tayari unaifahamu na kuiendesha siyo kusubiri hadi ustaafu unaweza kufa kwa presha kwani itakufa na kiasi chote cha fedha za mafao kitakwenda na maji”alisema
Kadhalika, aliwataka Watanzania kuchangamkia fursa zilizopo hivi sasa mkoani Dodoma ikiwemo uwepo wa Ikulu ya Chamwino, Bunge pamoja na mji wa serikali.
“Watu hatupaswi kuendelea kulalamika kuwa hali ni ngumu bali tutumie fursa ya uwepo wa ongezeko la watu mkoani hapa kufungua miradi kama hii ya migahawana na mingineyo ili kutoa huduma itakayokidhi mahitaji ya ongezeko hilo la watu mkoani hapa”alisema
Vile vile, alitoa ushauri kwa serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wazawa ikiwemo kuwapaunguzi riba kwenye mikopo ili wapate mitaji watakayo itumia kufanya uwekezaji mkubwa.
Hata hivyo, aliipongeza serikali ya awamu ya sita kupitia wizara ya Kilimo kwa ubunifu wa mradi wa jenga kesho iliyo bora (BBT) ambayo itasadia vijana kupatiwa mashamba, mbegu, mafunzo pamoja na nyenzo muhimu ambazo watakwenda kuzitumia ili kujikwamua kiuchumi.
No comments:
Post a Comment