Kampeni kutokomeza ukeketaji zapunguza vitendo hivyo Singida - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 13, 2023

Kampeni kutokomeza ukeketaji zapunguza vitendo hivyo Singida

Ofisa Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida, Shukrani Mbago (kulia) akigawa vipeperushi vya kuelezea madhara ya Uleketaji kwa wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Singida


Na Mwandishi wetu Singida

SHIRIKA lisilokuwa la Kiserikali la Woman Wake Up (Wowap) limesema kampeni mbalimbali zinazoendelea nchini zimeongeza uelewa wa wananchi juu ya madhara ya ukeketaji na hivyo kupunguza vitendo hivyo katika mkoa wa Singida.


Akizungumza kwenye mnada wa Njia panda ya Merya Halmashauri ya Singida Mratibu wa Wowap Nasra Suleiman alisema uelewa wa wananchi juu ya madhara ya ukekeaji umeongezeka.


Amesema kuwa wamekuwa wakifanya utekelezaji wa mradi wa kupinga vitendo vya ukeketaji , Mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Woman Actions Against FGM (WAAF) Japan na unatekelezwa na Shirika la Women Wake Up (WOWAP) Dodoma.


Amesema kuwa wamekuwa wakifanya kampeni ya kutokomeza ukeketaji wa wanawake na wasichana na kampeni hizo zinafanyika kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu ikiwemo minadani.


“Mnada wa njia panda ya Merya unakusanya watu wengi, tumefika na kutoa elimu hapa ,mwitikio ni mkubwa nawengi waliuliza maswali hasa kuhusiana na suala la adhabu,” amesema


Amesema kuwa sababu kubwa zinazopelekea ukeketaji ni sedtiri, dini, kuhifadhi utamaduni, kuhifadhi bikra, kuliunda heshima ya familia, kukubalika katika jamii hasa kuhusiana na ndoa,.


“Ukeketaji ni kinyume cha sheria pia ni kinyume cha sheria kumsaidia mtu yeyote kufanya ukeketaji wa namna yoyote,atakayepatikana na kosa la hatia ya kukuketaatafungwa na kutozwa faini,” alisema


Amesema kuwa hapa Tanzania katiba inakataza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, vitendo hatarishi ukeketaji ni kuvunja sheria za nchi.


“Mpango wa taifa wa utekelezaji wa kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na Watoto, wa mwaka 2017- 2018, 2021-2022 umeeleza kwa ufasaha kwamba ukeketaji ni mila inayoathiri wanawake na Watoto,” alisema

 
"Uelewa wa wananchi juu ya ukeketaji umeongezeka," alisema.

 
" Tumekuwa tukitoa elimu.katika maeneo.mbalimbali kwa wananchi Ili waache vitendo vya ukeketaji,jamii inatakiwa ipewe elimu ya kutosha ili iweze kutokomeza mila hiyo," alisema.


Mkazi wa Merya, Asha Senge (60) alisema kuwa vitendo vya ukeketaji vimepungua sana tofauti na miaka ya nyuma.


“Siku hizi ni tohara tu kwa Watoto wa kiume, Watoto wa kike watu wanaogopa kuwagusa watafungwa,” alisema


Amesema kampeni za kupinga ukatili n ahata ukeketaji zimesaidia sana kuongeza uelewa wa wananchi.

No comments:

Post a Comment