Na Okuly Julius-Dodoma
Mradi huo wa kila Binti Asome unaolenga kuboresha upatikanaji wa fursa za elimu na ujuzi kwa mabinti wa Tanzania kukuza uwezeshwaji wake na kupata fursa za ajira staha, itachangia kuongeza viwango vya uhitimu kwa wasichana katika shule za sekondari,
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa na Waziri mwenye dhamana ya Shirika la Maendeleo ya Uchumi la Pasifiki la Canada, Mhe.Harjit Sajjan, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda.
Pamoja na mambo mengine ziara hiyo inayolenga kutembelea miradi ya elimu inayofadhiliwa na Serikali ya Canada, amesema wote wanafahamu changamoto za kujifunza na kukuza ujuzi zinazowakabili mabinti wa Tanzania Bara na Zanzibar.
CHAMNGAMOTO ZINAZOWAKABILI MABINTI.
Akizungumzia changamoto za kujifunza na kukuza ujuzi zinazowakabili mabinti wa Tanzania Bara na Zanzibar, Sajjan amezitaja kuwa ni pamoja na tofauti za kimuundo, mzigo wa kazi za nyumbani na majukumu ya uangalizi wa familia, ukatili wa kijinsia.
Nyingine ni mitazamo na desturi za kimila, ikiwemo ndoa na mimba za utotoni, pale elimu ya wasichana inapochukuliwa kuwa ya thamani ndogo, hakuna motisha kwao kumaliza masomo, Kwa kuongeza, ni ukweli kwamba shule nyingi hazikidhi mahitaji ya wasichana walio katika kipindi cha balehe.
Waziri huyo alizitaja changamoto nyingine kuwa ni, si kwa suala la usalama, au upatikanaji wa Maji au vyoo Maalum vya kuhifadhi wakati wa hedhi, wasichana wote wanapaswa kupata fursa ya elimu na wasichana wote wanapaswa kupata fursa ya kumaliza masomo yao bila kujali hali zao.
"Tunaipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada zake kuwezesha upatikanaji wa elimu, tunawapongeza kwa maendeleo makubwa katika ngazi ya elimu ya msingi ambapo usawa wa kijinsia umefanikiwa, tunampongeza juhudi za kuondoka marufuku ya mabinti wenye ujauzito na mabinti waliojifungua kurejea shuleni,"amesema Sajjan
Amesema Canada imekuwa mshiriki wa muda mrefu wa Tanzania katika sekta ya elimu, wameshiriki kuboresha viwango vya elimu, na upatikanaji wa elimu, kwa shule zote za msingi na sekondari kwa wasichana na wavulana.
Waziri Sajjan kwa kushirikiana na serikali, Canada imewekeza katika mafunzo madhubuti kwa walimu wa baadaye katika Vyuo 36 vya ualimu, katika kipindi cha miaka 14 iliyopita, Canada imetoa zaidi ya dola Milioni 250 za kwenye mfumo wa elimu.
"Niko hapa kudhibitisha kwamba Canada itaedelea kusaidia jitihada za elimu nchini Tanzania, kama Mwalimu, Julius Nyerere alivyosema, "elimu sio njia ya kuukimbia umasikini, ni nyenzo ya kupambana nao,"alinukuu Waziri huyo.
MIRADI KUWEZESHA ELIMU
Kudhibitisha ishirikiano huo ndio leo Canada inatangaza dola za Canada Milioni 25 Kwa mradi wa kila Binti Asome Tanzania Bara na Zanzibar chini ya UNICEF, utakaowezesha elimu kwa mabinti katika ngazi ya msingi sekondari, haswa katika masomo ya hisabati na Sayansi.
Mradi huo wa kila Binti Asome unaolenga kuboresha upatikanaji wa fursa za elimu na ujuzi kwa mabinti wa Tanzania kukuza uwezeshwaji wake na kupata fursa za ajira staha, itachangia kuongeza viwango vya uhitimu kwa wasichana katika shule za sekondari,"amesisitiza.
Pia amesema italenga kuwawezesha mabinti, wenye umri kati ya miaka 10 na 19, kujifunza na kuongeza ujuzi wao ili kuendana na mahitaji ya soko ya sasa na ya baadaye nchini Tanzania na itatoa fursa za upatikanaji wa njia Bora mbadala za kujifunza kwa mabinti wajawazito na wasichana waliojifungua ambao wemeenguliwa kwenye mifumo rasmi ya elimu.
Kuhusu kutangaza dola za Canada Milioni 25 kwa ajili ya mpango wa Ajira kupitia ujuzi kwa elimu ya UFUNDI stadi, alisema mradi huo unatekelezwa na Shirika la Vyuo na Taasisi za Canada,unalenga kuhamasisha njia mbadala za elimu Kwa wanawake na wasichana.
Pia amesema unalenga kuboresha upatikanaji wa ujuzi wa biashara na mafunzo ya haki za binadamu katika jamii zao, utatoa usaidizi baada ya mafunzo ili kusaidia kipindi cha mpito baada ya kuhitimu Hadi kuajiriwa au kujiajiri.
"Mradi wa uwezeshwaji kupitia Program za ujuzi unalenga kuongeza ushiriki wa kiuchumi kwa wanawake na mabinti Tanzania kwa kuimarisha uwezo wa Vyuo vya maendeleo 12 na mashirika ya kijamii 16 kutengeneza na kutoa mafunzo ya ujuzi Kwa wanawake na mabinti,"amesema Waziri huyo wa Canada.
Awali Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema mahusiano haya yatasaidia kuendeleza mabadiliko ya elimu hapa nchini.
"Tumekuwa na mahusiano mazuri na nchi ya Canada katika masuala ya elimu, tunataka kuendelea kupeleka watanzania kusoma nchini Canada, wapo wengi wamesoma nchini humo, ushirikiano wetu ni mkubwa na tunauendeleza,"amesisitiza Profesa.Mkenda.
Pia amesema kupitia miradi na Fedha hizo wanazopatiwa na nchi ya Canada wanakwenda kufanya mabadiliko makubwa kwenye Vyuo vya ufundi nchini.
No comments:
Post a Comment