DODOMA NA SINGIDA YADHAMIRIA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, July 31, 2023

DODOMA NA SINGIDA YADHAMIRIA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI.


Na Okuly Julius-Dodoma

Tafiti zinaonesha Mkoa wa Dodoma na Singida imeendelea kuathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuathiri uzalishaji wa mazao ya kilimo mifugo na uvuvi.


Mikoa hiyo imedhamiria kusambaza mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa Mazingira.


Hayo yameelezwa leo julai 31,2023 Jijini Dodoma na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sherehe na maonyesho ya nane nane Kanda ya kati ambapo amesema mbinu hizo ni pamoja na mbinu za hifadhi ya maji na udogo mashambani.


"Mikoa ya Dodoma na Singida imeendelea kuathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuathiri uzalishaji wa mazao ya kilimo mifugo na uvuvi. Hivyo, Maonesho ya mwaka huu yameandaliwa kutoa ujumbe ambao utawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi kuhimili mabadiliko haya". amesema Senyamule.


Aidha,Senyamule amesema watajikita zaidi kusambaza teknolojia za kisasa katika kilimo na ufugaji bora ambapo Taasisi za utafiti za kilimo, mifugo na uvuvi zitashiriki maonesho hayo kuonesha teknolojia mbalimbali zilizozalishwa kwenye vituo vya utafiti na kuwawezesha wakulima kunufaika na elimu ya uzalishaji bora.


"Katika maonyesho ya mwaka huu Makampuni na watu binafsi wameleta teknolojia bora za ufugaji wa mifugo, mbegu bora za mazao mbalimbali kwa kuzingatia vipaumbele vya mkoa wa Dodoma na Singida. Taasisi za utafiti za kilimo, mifugo na uvuvi zinashiriki maonesho hayo kuonesha teknolojia mbalimbali zilizozalishwa kwenye vituo vya utafiti na kuwawezesha wakulima kunufaika na elimu ya uzalishaji bora". amesema Senyamule.


Sambamba na hayo, Senyamule ametaja matukio muhimu ya Maonyesho ya nane nane 2023 ikiwemo kongamano la Tasnia ya Alizeti,kongamano la zao la mtama,siku maalumu ya uhamasishaji uzalishaji kuku wa kienyeji pamoja na Tamasha la mashindano ya nyama choma.


"Mikoa ya Dodoma na Singida ilikabidhiwa jukumu la kuzalisha alizeti kwa wingi ili kupunguza nakisi ya mafuta ya kula nchini na hivyo kuokoa fedha za kigeni zinazotumika katika uagizaji wa mafuta ya kula nje ya nchi na Mikoa hii iliandaa mikakati ya utekelezaji na hali inaonyesha kuongezeka kwa upatikanaji wa mafuta ya kula na bei kushuka kutoka shilingi 7,000 kwa lita na sasa ni wastani wa shilingi 4,000 kwa lita". amesisitiza Senyamule.


Kauli mbiu ya Maonesho na Sherehe za Nane Nane Kitaifa kwa mwaka 2023 ni; “Vijana na Wanawake ni Msingi imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula” ambapo Kaulimbiu ya Kikanda ni “Kilimo ni Biashara, Biashara ni Uwekezaji”


No comments:

Post a Comment