Mkurugenzi wa Huduma za USafiri kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi - Sekta ya Uchukuzi Mhandisi Aron Kisaka akiongoza kikao Cha majadiliano ya pamoja kati ya Wawakilishi kutoka LATRA na baadhi ya Wamiliki wa vyombo vya usafirishaji Kwa njia ya Barabara na Viongozi wa vyama vya Ushirika wa wamiliki wa vyombo vya usafirishaji Kwa njia ya Barabara wa Mkoa wa Mwanza, kilichofanyika kwenye Ukumbi Mdogo uliopo kwenye Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mkoani humo Tarehe 22 Julai,2023
Lengo la kikao hicho Cha majadiliano ni kujengeana uelewa wa pamoja na kuandaa mifumo imara na endelevu ya usafirishaji Kwa njia ya Barabara mkoani Mwanza itakayojisimamia yenyewe Kwa miaka mingi na kuondoa Migogoro na mivutano ya mara Kwa mara inayoweza kujitokeza kati ya Wasafirishaji na Serikali ya Mkoa huo.
No comments:
Post a Comment