Halmashauri zatakiwa kutumia Mpango wa matumizi bora ya ardhi kukabili migogoro ya ardhi na mipaka ya vijiji - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 19, 2023

Halmashauri zatakiwa kutumia Mpango wa matumizi bora ya ardhi kukabili migogoro ya ardhi na mipaka ya vijiji

Katibu tawala halmashauri ya wilaya ya Mbinga Pendo Ndumbaro akifungua mkutano wa wadau kujadili rasimu ya mpango wa matumizi bora ya ardhi uliondaliwa na mradi wa uboreshaji usalma wa milki za ardhi(LTIP)


Na Mwandishi wetu -Dodoma 

KUTOKANA na ongezeko la migogoro ya ardhi na mipaka ya vijiji nchini ambayo imekuwa akisababisha baadhi ya maeneo kuwepo kwa matukio ya mauaji ya wakulima na wafugaji serikali imezishauri halmashauri kutumia Mpango wa matuzi bora ya ardhi kukabiliana na hali hiyo.


Katibu Tawala wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga, Pendo Ndumbaro alisema hayo jana wilayani hapa, alipokuwa akifungua mkutano wa wadau kujadili rasimu ya Mpango wa matumizi ya ardhi uliondaliwa na mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi (LTIP) kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo.


“Nipende kuchukua fursa hii kutoa shukrani za dhati kwa halmashauri ya wilaya ya Mbinga kwa jitihada ilizozifanya katika kufanikisha rasimu ya mpango huu wa matumizi ya ardhi.


“Mmeshirikiana vyema na watalaam kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, mmetoa rasilimali watu na vitendea kazi kama magari na ofisi hata kama mnavyo vichache lakini hamkusita kutoa ili kufanikisha jambo hili”alisema

Aidha, alitoa wito kwa jamii kuendelea kushirikiana na wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi na halmashauri ya wilaya ya Mbinga katika utekelezaji wa hatua zingine zinazofuata kwenye utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa milki salama za ardhi.


Alisema hatua hizi ni pamoja na kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa vijiji, upimaji wa vipande vya ardhi na kutoa hatimiliki za kimila.

“Napenda kushauri kuwa Mpango huu utumike kumaliza migogoro ya matumizi ya ardhi na migogoro ya mipaka ya vijiji, Mpango huu ukawe dira ya Matumizi sahihi ya kila kipande cha ardhi ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Mbinga”alisema


Kadhalika alisema Mpango huo uanishe na kutoa njia sahihi za kusimamia utunzaji wa maeneo ya hifadhi za vilele vya milima, misitu na vyanzo vya maji pia kuweka maeneo ya kimkakati ya uwekezaji kutokana na rasilimali zilizopo ndani ya halmashauri ya wilaya ya Mbinga.


“Pamoja na lengo hilo kuu, uandaaji wa Mpango wa matumizi ya ardhi ya halmashauri ya wilaya una malengo yenye tija kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa taifa letu kama vile kufungua fursa za uwekezaji, kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi na migogoro ya mipaka, kuhifadhi mazingira na mwisho kuboresha usalama wa milki za ardhi”alisema


Hata hivyo, alisema Mpango huo ni wa miaka 20 kuanzia mwaka huu 2023 hadi 2043 ukiwa na lengo kuu la kusimamia matumizi ya ardhi na kuimarisha ukuaji wa uchumi wa watu wanaoishi katika halmashauri ya wilaya kwa kuwa na matumizi endelevu ya rasilimali ardhi na kuzingatia uhifadhi wa mazingira.

No comments:

Post a Comment