Na Selemani Kodima
Mbunge wa Jimbo la Bahi Mhe.Keneth Nolo ameahidi kumalizia ujenzi wa madarasa kwenye vitongoji vya Chihundiche na Iyumba katika kata ya Nondwa kwa kutoa shilingi milioni 37.5 kwa ajili ya umalizaji na ujenzi wa madarasa hayo.
Keneth Nolo ameyasema hayo July 18 wakati alipofanya ziara katika kata ya Nondwa, ndani ya vitongaji vya Chihundiche na Iyumba huku lengo ni kufanya mikutano ya hadhara, kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wananchi hao.
Mbunge huyo amesema milioni 12 na Laki tano ni kwa ajili ya kumalizia madarasa katika Kitongoji cha Chidundiche ambapo shule hiyo ni mpango kupunguza umbali wa wanafunzi kwenda kufuata shule ya mama ya Nondwa .
Aidha ametoa ahadi kwa wakazi wa kitongoji cha Iyumba kuwapa milioni 25 kwa ajili ujenzi wa Madarasa mawili na kufanya kitongoji hicho kuwa na madarasa saba .
Kwa upande wa Maji ,Mhe ,Nolo amewahakikishia wakazi wa kitongoji cha Chihundiche kuwachimbia kisima cha maji ambapo tayari mkandarasi wa uchimbaji wa kisima hicho ameshapatikana na mwezi wa nane mwaka huu anategemea kuanza mchakato wa uchimbaji wa kisima hicho.
Kwa Kitongoaji cha Iyumba amewakikisha kushirikiana nao katika usambazaji wa mtandao wa bomba za maji baada ya kitongoji hicho kuanza kufaidika na kisima cha Maji lakini kukosekana kwa vituo maji katika maeneo yote imesababisha uwepo wa changamoto.
Wakati huo huo amewataka wananchi wa vitongoji hivyo kuacha kujenga mbali mbali hali itasababisha wakazi wengi kushindwa kuunganisha umeme pindi mradi wa umeme utakapokamilika ndani ya vitongoji hivyo.
Mhe,Keneth Nolo ambaye aliongozana na Meneja wa Mradi wa REA wilaya ya Bahi aliwahakikishia wakazi hao kuwa mpango wa kuunganishwa na Mradi huo sio stori tena Bali ni Vitendo vitaanza kufanyika ili kutekeleza ahadi yake ya kuhakikisha maeneo hayo yanafikiwa na nishati ya umeme.
Hata hivyo amewataka wakazi wa kitongoji cha Iyumba kujiandaa pindi umeme huo utakapoingia katika maeneo yao kuanganisha na kutumia kwa fursa ya kiuchumi.
Kwa upande wa Kilimo,Mbunge wa Bahi Mhe.Keneth Nolo amewataka wananchi kuwekeza nguvu zao katika kilimo na kila mwananchi kutenga Ekari 2 kwa ajili ya zao la mtaa ili kukabiliana na mabidiliko ya tabianchi ambapo imesababisha uwepo wa tatizo la ukosefu wa chakula chakutosha .
Nao Baadhi ya Viongozi wa kata hiyo Akiwemo Diwani wa kata ya Nondwa Mussa Lumondi ,Mwenyekiti wa Nondwa Bw Majuto Benard wamempongeza Mbunge huyo kwa kuanza ziara yake katika kijiji hicho na kutoa nafasi ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu ya haraka.
Wamesema yapo mabadiliko ambayo yamechangiwa na mbunge huyo ,kuanzia Elimu ,Maji,miundombinu ya barabara na katika upatikanaji wa chakula katika kipindi cha upungufu wa chakula katika kata hiyo.
Mbunge huyo ameanza Ziara yake ikiwa ni muendelezo wa ufatiliaji na utatauzi wa baadhi ya changamoto zinazowakumba wananchi wake kuanzia Ngazi ya vitongoji ,kijiji hadi kata na kutoa majibu kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali wa serikali ambao amekuwa akiongozana nao.
No comments:
Post a Comment