Na Okuly Julius-Dodoma
JESHI la Kujenga Taifa (JKT) katika Mwaka wa fedha wa 2023/2024, limetengewa kiasi cha Sh. biloni 9.96 kwa ajili ya kujenga miundombinu na kuongeza kambi zingine kwa ajili ya kuongeza idadi ya vijana wanaopatiwa mafunzo kwa mujibu wa sheria, wale wa mkataba pamoja na wale wa mafunzo ya hiyali.
Hayo yamebainishwa leo Julai 27,2023 Jijini Dodoma na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya JKT na mwelekeo wake katika mwaka wa fedha 2023/2024.
“Tunaishukuru sana serika yetu kwa kututengea kiasi hicho cha bilioni 9.96 kwa ajili ya kuboresha miundombinu yetu ya makambi ili kusaidia kuongeza idadi ya vijana ambao wanapata mafunzo kila mwaka hasa hawa wa mujibu wa sheria wanaohitimu kidato cha sita kila mwaka”amesema Jenerali Mabele
Jenerali Mabele amesema kuwa katika kipindi cha mwaka jana JKT, ilipokea vijana waliohitimu kidato cha sita 26,000 na mwaka huu imepokea vijana 52,119 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 54.
Amesema kuwa wanaipongeza serikali kwa jitihada zake za kuongeza fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya makambi kila mwaka tangu mwaka 2021/22 ambapo ilianza kutenga kiasi cha Sh. bilioni 3.27.
“Mwaka 2022/23 serikali ilitupatia kiasi cha Sh. bilioni 7.5 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu na kiasi hichi kilikuwa ni mara mbili ya kile kilichopita na hii inaonyesha azma ya serikali kuwezesha vijana wengi kupata mafunzo”amesema
Jenerali Mabele,amesema kuwa katika kutekeleza azma ya Rais Samia Suluhu Hassan ya Tanzania kuwa kapu la chakula katika bara la Afrika wameweka mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula.
Amesema katika mwaka huu wa fedha kiasi cha Sh. biloni nne kimetengwa kwa ajili ya kujenga miundombinu ya umwagiliaji ili kuongeza maeneo ya kilimo na uzalishaji ili kukidhi hitajhio la chakula kwa vijana na usalama wa chakula kwa taifa.
Hata hivyo ametoa wito kwa vijana nchini kuchangamkia fursa za mafunzo zinazotolewa na jeshi hilo ili kujipatia ujuzi wanaoweza kuutumia mra watakapo maliza mkataba wao wa miaka miwili ya kulitumikia Jeshi hilo.
“Hivi sasa tunazungumza na wizara ya Kilimo kuona ni kwa jinsi gani ule mradi wa Jenga kesho iliyo bora (BBT), kuunganishwa na vijana wanaohitimu mafunzo ya JKT ili kuwasaidia kupata shughuli za kufanya pindi wanapomaliza mikata yao ya miaka miwili na kukosa nafasi ya kuajiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama nchini”amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, amelipongeza jeshi hilo kwa namna linavyotoa mafunzo ya uzalendo kwa vijana na makundi mengine nchini.
“Meja Jenerali Mabele, niwapongeze kwa kazi nzuri manayoifannya na mimi nitazungumza na vyama vya waandishi wa habari nchini kuona ni kwa namna gani tunaweza kuwapeleka JKT waandishi wetu waje wajifunze ili kuwa wazalendo watakapotoka huko hata karimu zao zitakuwa na uzalendo mwingi na taifa lao”amesema Msigwa
No comments:
Post a Comment