Na.Samwel Mtuwa - GST
Utafiti umebaini kuwa Mkoa wa Dodoma una aina nyingi za madini kulinganisha na mikoa mingine nchini.
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za madini zilizofanywa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania(GST) zimeonesha kupitia kitabu kipya cha madini yapatikanayo Tanzania.
Hayo yamebainishwa leo tarehe 28/7/2023 na Kaimu Meneja wa sehemu ya jioloji GST Maswi Solomon wakati akikabidhi kitabu cha Madini Yapatikanayo Tanzania toleo la tano kwa mkuu wa mkoa Dodoma Bi. Rose Senyamure.
Hayo yamesemwa na Mtaalam kutoka GST Bw. Maswi Solomon wakati akikabidhi Kitabu cha Madini Yapatikanayo Tanzania toleo la Tano kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.
Akieleza sababu za mkoa huo kuwa na aina mbalimbali za madini Maswi amesema kuwa ni kutokana na Mkoa wa Dodoma kuwa kwenye Ukanda maalum wa jiolojia unaupitiwa na mabadiliko tofauti ya kijiolojia na kuufanya kuwa na orodha ya madini mengi ya aina mbalimbali kuliko Mikoa mingine yote ukifuatiwa na Mkoa wa Morogoro na Lindi.
Maswi alieleza kuwa baadhi ya madini hayo ni madini mkatakati kama vile Lithium, Nikel, Chuma, Urani, Shaba na Helium.
Aidha, baadhi ya madini mengine ambayo yametambuliwa kuwa Muhimu kwenye matumizi ya viwanda vya ndani ni pamoja na madini ya Chokaa, Jasi, Feldspar, Mfinyanzi, Quartz na Kyanite.
Madini mengine ambayo ni ya kipekee kwa sasa yanapatikanayo Tanzania tu ambayo ni madini ya Yoderite ambayo yako katika Mlima wa Mautia Wilaya ya Kongwa Mlima ambao GST imeshauri uhifadhiwa kwa ajili ya utalii wa jiolojia ikiwemo watafiti na wanafunzi kujifunzia na kushuhudia madini hayo.
Kitabu hiki kimekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Waziri Mkuu alilo litoa akiwa Mwanza kwenye Mkutano wa Femata mwaka 2023.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameipongeza GST kwa jitihada za kutangaza fursa za madini nchini na kuahidi kutumia taarifa hizo kwa kuvutia uwekezaji katika mkoa wa Dodoma ambao unaongoza kwa wingi wa aina mbalimbali za madini.
No comments:
Post a Comment