MPANGO WA KUTOA MAJI ZIWA VICTORIA UPO PALE PALE- MHANDISI ARON - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, July 28, 2023

MPANGO WA KUTOA MAJI ZIWA VICTORIA UPO PALE PALE- MHANDISI ARON

Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph akieleza utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2023/24 katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo Julai 28, 2023, jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma

SERIKALI imesema itaendeleza azma yake ya kutoa maji kutoka ziwa Victoria mkoani Mwanza na kuyapeleka Dodoma ili kukabili upungufu uliopo sasa na kukomesha mgao unaoendelea.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Mhandisi Aron Joseph, ameyasema hayo Leo Julai 28,2023 ,jijini Dodoma, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo na mwelekeo wa mwaka wa fedha 2023/2024.


Mhandisi Joseph, amesema mpango wa serikali kuyatoa maji katika ziwa hilo haujabadilika kwakua ni moja kati ya mikakati ya kitaifa ya kukabiliaana na shida ya maji kufuatia ongezeko kubwa la maji mara baada ya serikali kuhamia Dodoma.


"Mipango ya muda mrefu ya kukabiliaana na hali hii ya shida ya maji katika mkoa wa Dodoma ni pamoja na kuleta maji ya ziwa Victoria mkoani Mwanza kuja kutatua kero hii ya ongezeko la mahitaji ya maji ambapo kiasi cha Sh. trioni 1.2 zinahitajika kwa ajili ya mifumo ya kusafirisha maji "amesema Mhandisi Joseph



Amesema mpango mwingine wa muda mrefu ni pamoja na ujenzi wa bwawa la Farkwa wilayani Chemba, ambapo zaidi ya sh.biliomi 300 zinatarajiwa kutumika kukamilisha mradi huo.


Akizungumza kuhusu hali ya upatikani wa maji katika jiji la Dodoma amesema hivi sasa mahitaji ya maji kwa siku ni lita milioni 133.4 ambapo uwezo kuzalisha ni lita milioni 68.7.


"Uzalishaji wa maji hivi sasa katika jiji letu la Dodoma ni asilimia 50 ya mahitaji hivyo upungufu uliopo ni lita milioni 64, hali ambayo inatulazimu kutoa huduma zetu kwa mgao wa masaa 13 kila siku na mgao huu unawafikia asilimia 91 ya watu wote wa jiji la Dodoma"amesema Mhandisi Joseph


Aidha, amesema ili kukabiliana na hali hiyo wanaendelea na mikakati mbalimbali ikiwemo uchimbaji wa visima katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma ikiwemo eneo la Kata ya Nzuguni.


Hata hivyo amesema mikakati mingine ni kuanzia ujenzi wa miundombi ya huduma ya maji taka ikiwemo ujenzi wa mabwawa pamoja na mifumo ambayo itasaidia kumaliza kero iliyopo sasa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma.

No comments:

Post a Comment