NIRC KUCHIMBA MABWAWA 100 KWA AJILI YA UMWAGILIAJI NCHINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, July 28, 2023

NIRC KUCHIMBA MABWAWA 100 KWA AJILI YA UMWAGILIAJI NCHINI

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Raymond Mndolwa akieleza utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo Julai 28, 2023, jijini Dodoma.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimfuatilie Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Raymond Mndolwa wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 leo Julai 28, 2023, jijini Dodoma.


Na Okuly Julius-Dodoma

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imejipanga katika Mwaka huu wa fedha wa 2023/24 ,kujenga mabwawa 100 nchi nzima ili kusaidia wakulima kuweza kulima zaidi ya vipindi viwili Kwa Mwaka hivyo kufanya Jumla ya Mabwawa kuwa 114 ambayo yatawasaidia wakulima kuwa na Kilimo Cha uhakika.


Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Bw.Raymond Mndolwa ameeleza hayo leo Julai 28,2023 wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wake Kwa Mwaka huu wa fedha.


Katika Mwaka wa Fedha 2023/2024, mwelekeo wa Tume ni kuendelea kutekeleza miradi itakayoongeza eneo la umwagiliaji lenye ukubwa hekta 256,185.46 ili kufikia hekta milioni 1,200,000 kama ilivyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2020),


"Katika mwaka huu wa Fedha tutakarabati miundombinu ya umwagiliaji katika Skimu 24 zenye jumla ya hekta 32,092; kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa mabwawa mapya 100 yenye wastani wa mita za ujazo 936,535,700 na kuanza ujenzi wa mabwawa hayo,"amesema Mndolwa


Ambapo amebainisha kuwa katika Awamu ya Tatu ya Mpango Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP III; 2021/2022-2025/2026) na Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP II) na kufikia hekta milioni 8.5 ifikapo 2030 (Agenda 10/30).


Ili kufikia malengo hayo Tume imepanga kutekeleza jumla ya miradi 822, ambapo miradi 114 ni ya ujenzi wa mabwawa na 103 ni ya ujenzi na ukarabati wa skimu za umwagiliaji.


Pia amezungumzia maeneo ya kipaumbele katika Mwaka wa Fedha 2023/2024. Kukamilisha ujenzi wa skimu mpya 25 zilizoanza kutekelezwa katika Mwaka 2022/2023, kukamilisha ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji katika skimu 30 zilizoanza kutekelezwa katika Mwaka 2022/2023;


Pia Tume hiyo itakamilisha ujenzi wa mabwawa 14 yenye mita za ujazo 131,535,000 yaliyoanza kujengwa Mwaka 2022/2023, kukamilisha usanifu wa mabonde 22 ya Umwagiliaji ulioanza Mwaka 2022/2023;


Mkurugenzi huyo amesema kuwa tume hiyo itaanza ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji kwenye mabonde 22 yenye jumla ya hekta 306,361, kuanza ujenzi wa skimu mpya 35 zenye jumla ya hekta 111,390;


Kukarabati miundombinu ya umwagiliaji katika Skimu 24 zenye jumla ya hekta 32,092; kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa mabwawa mapya 100 yenye wastani wa mita za ujazo 936,535,700 na kuanza ujenzi wa mabwawa hayo.


Kujenga miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba ya pamoja (Block farms) yenye jumla ya hekta 79,518.46 katika Mikoa ya Kigoma, Njombe, Mbeya, Kagera na Dodoma kupitia programu ya Building Better Tomorrow (BBT);


Amesema Uhakika wa Maji ya umwagiliaji Kwa Wakulima yataenda kijibu kile kilimo cha kilima mara mbili kwa mwaka bila changamoto yoyote kwa kuwa mabwawa hayo yatakuwa bora nayauhakika na kuongeza kilimo hicho kitakuwa ni kilimo chenye tija nakisaidia kukuza uchumi katika jamii


Pamoja na hayo ameeleza kuwa tume hiyo pia imejipanga kutumia Teknolojia katika kuhakikisha wanaboresha upatikanaji wa Maji na kuwasaidia wakulima kuwa na uhakika wa Maji Kwa misimu yote.


Mndolwa ametoa wito Kwa wakulima kulipa ada ili kuendelea kuboresha Mazingira ya kilimo Cha umwagiliaji hapa Nchini.


"Nitumie Fursa hii kuwaomba wakulima kulipa ada wachangie maendeleo ya Tume ili tuweze kuwahudumia Kwa uhakika,"amesema Mndolwa


Ili kutekeleza maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa na Tume hiyo imeidhinishiwa na Bunge kiasi cha Shilingi 373,511,998,000/= kwa ajili ya mwaka wa fedha 2023/2024,ambapo Kati ya Fedha hizo, miradi ya maendeleo Shilingi 299,964,223,000 /= (80.3%) na, matumizi ya Kawaida Shilingi 73,547,775,000 (19.7%).

No comments:

Post a Comment