Na Okuly Julius-Dodoma
MAMLAKA ya Udhibiti Ununuzi wa Umma PPRA imesema kukosekana Kwa uwazi katika mchakato wa ununuzi wa umma kunasababisha changamoto za upatikanaji wa taarifa za zabuni, thamani ya mkataba na kusababisha ukosefu wa uaminifu na Imani kwa Taasisi za Umma pia hata wananchi wanakosa Imani kwa Serikali kutokana na Matumizi yasiyoeleweka.
Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Eliakim Maswi wakati,akieleza utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wake katika Mwaka wa Fedha 2023/24 katika mkutano na Waandishi wa Habari leo Julai 17, 2023 Jijini Dodoma.
" Ukosefu wa uwazi katika mchakato wa Ununuzi wa Umma kunasababisha Changamoto za upatikanaji wa taarifa Hali inayopelekea kukosekana kwa Imani kwa taasisi za Umma pia wananchi kukosa Imani na serikali Kutokana na Matumizi yasiyoeleweka," Amesema Mtendaji Maswi.
Pia amebainisha kuwa Mamlaka hiyo imekuwa ikikabiliwa na hatari kubwa ya rushwa kwa Watendaji na maafisa serikalini kwa kutoa mikataba au kuwapa faida zisizo halali wazabuni wasio na sifa.
"Kumekuwepo na viashiria vya vitendo vya rushwa katika mchakato wa Ununuzi wa Umma hali inayopunguza ushindani na kusababisha upotevu wa fedha za Umma,"
Na kuongeza kuwa " Wanao hisiwa na kulalamikiwa kuwa wanajihusisha na vitendo hivyo viovu vya rushwa ni pamoja na Watendaji na maafisa waliomo serikalini," ameeleza Maswi.
Ameeleza Changamoto nyingine ni pamoja. Na mchakato wa zabuni kuchukua muda mrefu ambapo Amesema ,Ni takwa la kisheria kufuata taratibu na kanuni za Ununuzi wa Umma ikiwa ni pamoja na kufuata sheria za ushindani na taratibu zingine zinazohusiana nazo.
" Hatua hizi za kisheria Mara nyingi huongeza muda wa mchakato wa Ununuzi Hata hivyo watumishi wasio waadilifu wanakuwa ndio sababu ya Zabuni kuchukua muda mrefu," Amesema
Pia Bw.Maswi amesema Serikali imeendelea kudhibiti Matumizi ya Fedha za Umma kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo mifumo ya kielektroniki ili kuleta tija na ufanisi unaostahili katika utekelezaji wa bajeti husika.
Amesema kwa mujibu wa sheria ya Ununuzi wa Umma ,Mamlaka imekasimiwa jukumu la kusanifu ,kuanzisha nakuhusisha mifumo mbalimbali ya kielektroniki kwa ajili ya kuweka uwazi na kuleta tija kwenye Ununuzi wa Umma.
"Kwa kuzingatia Changamoto zilizopo , Serikali ikifanya manunuzi ya kujenga Mfumo mpya unaojulikana kwa jina la " National e-procurement System of Tanzania (NeST) Mfumo unaopatikana kwa kupitia anuani ya https://www.nest.go.tz," Amesema Mtendaji hiyo.
Na kuongeza" Ifikapo Tarehe 1 Oktoba 2023 ,taasisi nunuzi zote za serikali hazitoweza kutumia mialiko ya Zabuni kwenye Mfumo wa TANePS na badala yake zitapaswa kutumia Mfumo wa NeST," Amesema Afisa Mtendaji Maswi.
Hata hivyo Amesema baada ya Tarehe hiyo Mfumo wa TANePS hautopatikana hewani kwa ajili ya Matumizi ya Ununuzi wa Umma isipokuwa kwa shughuli za ndani Kama kupata taarifa za Ununuzi.
Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) imeanzishwa kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa thamani ya fedha katika ununuzi na ugavi, kuhakikisha uzingatiaji wa haki, ushindani, uwazi, uendelevu, uwajibikaji, matumizi mazuri ya fedha, ufanisi na uadilifu katika ununuzi na ugavi.
Malengo mengine ya uanzishwaji ni kuweka viwango vya mifumo ya ununuzi wa umma na ugavi, kufuatilia uzingatiaji wa sheria wa Taasisi Nunuzi, kujenga uwezo katika ununuzi na ugavi katika Jamhuri ya Muungano kwa kushirikiana na Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma na Taasisi nyingine za kitaaluma.
No comments:
Post a Comment