Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Prof. Lazaro Busagala amesema TAEC imefanya mabadiliko makubwa katika katika kipindi cha muda mfupi kwa kuboresha eneo la teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ambapo sasa wafanyabiashara wanaosafisha vyakula wanapata vibali kwa wakati kutoa siku zaidi ya saba hadi muda wa saa moja hadi masaa matatu mtu anakuwa ameshapata kibali.
Prof. Busagala ameyasema hayo baada ya kutembelea banda ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania katika maonesho ya 47 ya kimataifa ya biashara maarufu kama SABASABA.
Aidha Prof. Busagala ameongeza kuwa TAEC imeongeza ofisi hadi 52 lengo likiwa ni kusogeza huduma karibu na wananchi.
TAEC inashiriki maonesho ya SABASABA kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi namna mionzi ilivyo na faida na jinsi gani TAEC inavyodhibiti matumizi holela ya mionzi.
No comments:
Post a Comment