RAIS SAMIA AMETOA FEDHA KUJENGA SHULE MPYA MAALUM ZA WASICHANA KILA MKOA: DKT. MSONDE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, July 16, 2023

RAIS SAMIA AMETOA FEDHA KUJENGA SHULE MPYA MAALUM ZA WASICHANA KILA MKOA: DKT. MSONDE


OR -TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu), Dkt. Charles Msonde amesema Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari imetoa fedha za kujenga Shule mpya maalum za Sekondari za Bweni na sayansi kwa ajili ya wanafunzi wa kike katika mikoa yote nchini.


Dkt. Msonde ameeleza hayo katika ziara yake ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya elimu na hali ya utoaji wa elimu nchini katika halmshauri za wilaya ya Hanang, Babati na Babati Mji mkoani Manyara.



Amesema kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) wa miaka mitano, Serikali imetenga Shilingi Trilioni 1.2 utajenga shule mpya za Sekondari 1,026 kati ya hilo shule 26 ni shule Maalum za wasichana zinazojengwa moja kila mkoa.


“kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari kila mkoa unapewa bilioni 4 kwa awamu mbili kujenga shule ya wasichana ya bweni ambayo itakuwa na Uwezo wa kupokea wanafunzi 1,080 na kidato cha kwanza hadi cha sita”



Dkt. Msonde amesema katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 Serikali ilipeleka shilingi bilioni 30 kwenye mikoa 10 ambapo kila mkoa ulipokea Bilioni 3 za awamu ya kwanza kwa ajili ya kujenga shule za Sekondari za wasichana.


Aidha, Dkt. Msonde amesema Katika mwaka wa fedha 2023/23, Serikali tayari imepeleka fedha katika mikoa 16 iliyosalia ambapo mikoa yote 26 nchini inaendelea na utekelezaji wa shule hizo ambazo mwakani zitakuwa zimekamilika na kuanzq kupokea wanafunzi.



Kadhailika, amesema shule nyingine 1,000 za sekondari zinaendelea kujengwa kwa awamu ambapo mwaka wa fedha wa 2021/22 zilijengwa shule 232 vile vile mwaka fedha ulioisha wa 2022/23 zimetolewa fedha kujenga shule nyingine za sekondari 212 ambazo zitakamilika ifikapo Agosti 2023.


No comments:

Post a Comment