Rais Samia Ataja Malengo Manne ya Afrika ya Miaka 40 Ijayo - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 26, 2023

Rais Samia Ataja Malengo Manne ya Afrika ya Miaka 40 Ijayo


Na Immaculate Makilika - MAELEZO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Bara la Afrika linahitaji mageuzi katika nyanja zote muhimu kwa ajili ya maendeleo ya bara hilo.

 

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akihutubia katika kilele cha mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

 

“Ni wazi kuwa Bara letu bado linahitaji mageuzi makubwa katika nyanja zote muhimu za uzalishaji na maendeleo. Na haya ndio malengo na madhumuni ya ajenda ya Maendeleo ya Afrika tunayoitaka ya mwaka 2063 ambayo imeweka malengo 7”, alieleza Mhe. Rais Samia.

 

Mhe. Rais Samia alisisitiza “Nataka nijielekeze kuyazungumzia malengo manne, ambayo ni Afrika ambayo mafanikio yake yanajikita kwenye ukuaji jumuishi wa uchumi na maendeleo endelevu, Bara lenye utangamano kisiasa kwa kuzingatia fikra za kimajumuishi na mwelekeo wa kimapinduzi, Afrika inayozingatia misingi ya utawala bora, demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria na Afrika ambayo maendeleo yake yanatokana na watu kwa kutumia vipaji vyao, hususan wanawake na vijana pamoja na kutoa makuzi bora kwa watoto”.



Zaidi ya watu 1,200 kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakiwemo Wakuu wa Nchi hizo, viongozi wa Serikali, Watumishi wa Umma, wadau, Waandishi wa Habari pamoja na wananchi wameshiriki Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu ulioanza Julai 25, 2023 na kumalizika Julai 26, 2023.

 

Mbali na masuala ya rasilimali watu hususan kwa vijana, mkutano huo ulizungumzia pia sekta ya elimu, afya, kilimo, fedha na sayansi na teknolojia ambapo zimejadiliwa kama wazalishaji wa rasilimali watu.

No comments:

Post a Comment