VIJANA WAHAMASISHWE KUSOMA MASOMO YA SAYANSI ILI KUCHOCHEA UCHUMI WA KIDIJITI-DKT.JABIR - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, July 18, 2023

VIJANA WAHAMASISHWE KUSOMA MASOMO YA SAYANSI ILI KUCHOCHEA UCHUMI WA KIDIJITI-DKT.JABIR

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Bakari akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wake Kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 katika mkutano na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Julai 18, 2023 , jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabir Bakari akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wake Kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 katika mkutano na Waandishi wa Habari leo Julai 18, 2023 , jijini Dodoma.


Na Okuly Julius-Dodoma

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema,ili kushiriki katika Ujenzi wa uchumi wa Kidijiti ni lazima kuhakikisha vijana wengi wa wakitanzania wanahamasishwa kusoma masomo ya Sayansi hususani Hisabati kwanzia ngazi za Chini.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo , Dkt. Jabir Bakari wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2023/24 katika mkutano na Waandishi wa Habari leo Julai 18, 2023, Jijini Dodoma.


"Tuna Mpango wa kuanzisha 'DIGITAL CLUBS' Kwa ajili ya kutoa Mafunzo Kwa vijana na watumiaji WA mitandao kwani Uchumi wa Kidijitali unahitaji Wataalam hivyo ili kufikia huko Kuna umuhimu wa kuwafanya vijana wetu wa Kitanzania kusoma masoma ya Sayansi ili tuwapate Wahandisi watakaosaidia kuendesha uchumi huu ambao unahitaji matumizi makubwa ya mtanzao,"amesema Dkt.Jabir


Dkt.Jabir amezungumzia mchango wa Sekta ya Mawasiliano katika ukuaji na undelezaji wa sekta nyingine ikiwemo kuleta ustawi wa maisha ya wananchi kisiasa, kijamii na kiuchumi.

“Kutokana na mchango huo, Sekta ya Mawasiliano imekuwa ya kimkakati na ya msingi katika maendeleo ya uchumi wa kidijiti na uchumi wa buluu nchini Tanzania, kuanzia ngazi ya mtu binafsi, ngazi ya kaya, Taasisi na kitaifa. Utoaji wa huduma za mawasiliano ni wa ushindani hivyo umesababisha kuongezeka kwa idadi ya mitandao, matumizi ya TEHAMA na aina za huduma zinazotolewa kwa Wananchi, Taasisi na Serikali kwa ujumla.”, alisema Dkt. Jabiri.


Pia Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa, kuenea kwa huduma hizo kunawezeshwa na uwepo wa sera imara, sheria nzuri na mifumo wezeshi ya kiusimamizi na utoaji leseni. Ambapo TCRA imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia malengo yaliyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa (FYDP III) kwenye sekta ya mawasiliano.


Dkt. Jabiri ameongeza kuwa utekelezaji wa Dira hiyo ya Taifa na Mpango wa Maendeleo unahusisha mchango wa TCRA kwenye uchumi kwa kuimarisha miundombinu ya mawasiliano na upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa lengo la kuboresha uchumi wa kidijiti na uchumi wa buluu.


Dkt.Jabiri amebainisha malengo mengine kuwa ya Mamlaka hiyo kuwa ni kuendelea kuweka mazingira bora ya ushindani kwenye sekta ya mawasiliano ili wananchi wengi waweze kumudu gharama za huduma za mawasiliano, kulinda watumiaji wa huduma za mawasiliano dhidi ya uhalifu mtandaoni kwa kutumia mifumo ya kiusimamizi, kugawa rasilimali za mawasiliano, ikiwa ni pamoja na masafa na kutoa leseni kwa watoa huduma zinazowezesha kuongeza idadi ya watumiaji wa intaneti ili kufikia lengo la asilimia 80 ifikapo 2025.


Amesema kuwa Tanzania inazidi kuendeleza mfumo jumuishi wa kifedha kutokana na kuongezeka kwa watumiaji wanaofanya miamala kupitia simu za mkononi ambapo takwimu za mawasiliano za mwezi Juni 2023 zinaonyesha kwamba huduma za pesa kupitia simu za mkononi
zimeongezeka.


"Akaunti za pesa kwa simu za mkononi zimeongezeka na kufikia
47,275,660 Juni 2023 kutoka akaunti 38,008,482 mwezi Julai 2022 ikiwa ni ongezeko la
24%. Idadi ya miamala imeongezeka kutoka 349,952,830 Julai 2023 hadi miamala 420,675,884
Juni 2023. Aidha, akaunti za pesa kwa simu zimeongezeka kwa 24% kuanzia Julai 2022
hadi Juni 2023; wakati miamala ikiongezeka kwa 20%,"amesema Dkt.Jabir


Kwa upande wa Sekta ndogo ya Uyltangazaji Dkt.Jabir amesema takwimu za utangazaji zinaonyesha kwamba visimbuzi 3,342,626 vilikuwa hewani hadi
Juni 2023 ikilinganishwa na visimbuzi 3,169,231 mwezi Julai, 2022. Kati ya hivyo,
1,700,205 ni vya dijitali kwa mfumo wa televisheni wa utangazaji wa mitambo ya ardhini (Digital Terestrial Television - DTT) na 1,642,421 ni vya mfumo wa televisheni wa satelaiti.


"Dar es Salaam inaongoza kwa kuwa na visimbuzi (1,286,354), ikifuatiwa na Arusha
(275,449), Mwanza (262,380) na Mbeya (208,924). Mikoa yenye visimbuzi vichache ni
Songwe (1,357).Televisheni za waya (Cable TV) zimeenea kutoka watu 16,786 waliounganishwa 2018 hadi 19,671 Juni 2023. Huduma ya televisheni kwa waya (yaani Cable TV) imeenea mikoa ya Kanda ya Ziwa; ambapo Mkoa wa Shinyanga unaongoza; ukiwa na jumla ya
waliounganishwa 2,803, ikifuatiwa na Mwanza, yenye 2,195 na ya tatu ni Kagera ikiwa
na waliounganishiwa 1,770. Mikoa yenye wateja wachache ni Kilimanjaro (130),
Morogoro (120) na Pwani iliyounganisha wateja 30,"amefafanua Dkt.Jabir


Shughuli za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinagusa wadau wakuu watatu ambao ni Serikali yenye jukumu la kutoa sera na sheria,watoa huduma wanaopewa leseni na masharti ya namna ya kutoa huduma husika, na watumiaji wa huduma za mawasiliano ambao
TCRA ina jukumu la kulinda maslahi yao kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma zenye
ubora, usalama na kwa bei nafuu.

No comments:

Post a Comment