Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (wa pili kushoto) akikabidhi nyaraka za pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga.
Benki ya CRDB imetoa zawadi ya Pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura anayefanya shughuli za Uwakala Ngokolo Mitumbani Mjini Shinyanga kutokana na kuwahudumia wateja wengi zaidi.
Akizungumza leo Jumanne Julai 18,2023 wakati wa kukabidhi Pikipiki hiyo, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana amesema katika kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa huduma ya CRDB Wakala, benki ya CRDB imetenga zawadi mbalimbali ikiwemo kamisheni za fedha, bodaboda, bajaji na gari kwa ajili ya kuwazawadia mawakala wake watakaowahudumia wateja wengi zaidi.
"Benki ya CRDB inampongeza sana Mr & Mrs Charles Zacharia Wambura kwa kuwa mfano bora wa Mawakala wanaofanya kazi vizuri. Bwana Charles Zacharia Wambura amekimbiza sana miamala. Tunakupongeza sana kwa ushindi huu",amesema Wagana.
Ameeleza kuwa kutokana na umuhimu wa Mawakala, benki ya CRDB imekuja na kampeni ya kuwazawadia mawakala watakaotoa huduma kwa wateja wengi zaidi ambapo Kampeni hiyo imeanza mwezi Aprili na itafanyika kwa muda wa miezi mitano na zawadi nyingi zitatolewa ambazo ni Kamisheni/bonasi, pikipiki 40, Bajaji 5 na mshindi wa jumla atapata Gari jipya aina ya Toyota Alphard.
"Lengo la kutoa zawadi hizi ni kuwapa Motisha Mawakala wetu, sisi tunaamini Mawakala ni sehemu ya Benki ya CRDB kwa sababu wanafanya mambo yote yanayofanyika ndani ya Benki ya CRDB ikiwemo kuweka fedha, kutoa fedha,kufungua akaunti, malipo ya serikali na hivi karibuni tumeongeza jukumu jingine la kukata bima",amesema Wagana.
"Kwa hiyo Mawakala wa CRDB wanatusaidia sana na wanafanya kazi kubwa ndiyo maana tukiwa tunaadhimisha miaka 10 ya CRDB Wakala tumeona tusiwaache hivi hivi tukaja na hizi zawadi ili iwe chachu kwa Wakala wetu wanaokimbiza miamala",ameongeza Meneja huyo wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Tabora, Geita na Kigoma.
Kwa upande wake, Meneja Mahusiano Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi anayeshughulika na Mawakala, Peter Kidagaa amesema huduma ya CRDB Wakala iliyoanzishwa mwaka 2013 na kutokana na umuhimu wa Mawakala ndiyo maana wameanzisha Kampeni hiyo ili kuwashukuru na kutambua mchango wao mkubwa ambao umefanikisha kuifikisha CRDB wakala kwa miaka 10.
"CRDB Wakala imekuwa ikikua mwaka hadi mwaka, hivyo tukiwa tunatimiza miaka 10 tumeona Mawakala wetu tusiwaache hivi hivi ndiyo maana tukasema Miaka 10 pamoja hatukuachi hivi hivi. Tunaangalia Wakala gani amefanya miamala mingi lakini pia amefungua akaunti nyingi. Mshindi wetu huyu wa leo Charles Zacharia Wambura aliyepata zawadi ya pikipiki siyo tu ameshinda Shinyanga bali ameshinda kati ya mikoa minne ya Shinyanga, Tabora, Geita na Kigoma. Tunampa pikipiki hii mpya, kadi ina jina lake na hatumpangii matumizi",amesema Kidagaa.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Luther Mneney ametumia fursa kuwasihi Mawakala wa Benki ya CRDB kuchangamkia Kampeni ya 10 na kitu kwa kufungua akaunti nyingi na kufanya miamala mingi zaidi.
"CRDB tunasema Mchongo kama wote kwa Wakala wetu, Mchongo upo Mtaani kwako! .Tuungane kusherehekea miaka 10 ya huduma ya CRDB Wakala kwa kushiriki promosheni hii ya 10 na kitu. Wakala unachotakiwa kufanya ni kukimbiza miamala uwezavyo ya wateja wako, walipie bili, wakatie Bima na kuwafungulia akaunti za Al-Barakah na akaunti nyingine ujiongezee nafasi ya kushinda Kamisheni hadi zaidi ya mara 3, Gari jipya aina ya Toyota Alphard, Bajaji 5, bodaboda 40",amesema Mneney.
Akipokea zawadi ya Pikipiki Wakala wa Benki ya Charles Zacharia Wambura akiwa na mkewe wanayeshirikiana naye kufanya kazi ya Uwakala Mary Festo Bukumba ameishukuru Benki ya CRDB kwa kutambua mchango mkubwa wanaotoa kwenye benki hiyo huku wakiahidi kuendelea kukimbiza miamala zaidi na kufungua akaunti nyingi zaidi.
Kwa upande wake, Wakala wa Benki ya CRDB Grace Joliga amempongeza Wakala huyo kwa ushindi akisema " Tulikuwa tunajua ni Stori tu au CRDB wanatoa zawadi kwa kujuana, lakini kumbe ni kweli wanatoa zawadi kwenye kwa wanaofanya vizuri, hii ni motisha nzuri na sisi wengine tunajitahidi kuhakikisha tunaongeza kasi".
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga leo Jumanne Julai 18,2023 katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga. Picha na Kadama Malunde 1 blog
Muonekano wa pikipiki iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga leo Jumanne Julai 18,2023 katika Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga
Meneja Mahusiano Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi anayeshughulika na Mawakala, Peter Kidagaa akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga
Meneja Mahusiano Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi anayeshughulika na Mawakala, Peter Kidagaa akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (wa pili kushoto) akikabidhi nyaraka za pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Meneja Mahusiano Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi anayeshughulika na Mawakala, Peter Kidagaa akifuatiwa na Mke wa Charles Zacharia Wambura (Mary Festo Bukumba). Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana (wa pili kushoto) akikabidhi funguo za pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura Mkazi wa Mjini Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Meneja Mahusiano Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi anayeshughulika na Mawakala, Peter Kidagaa akifuatiwa na Mke wa Charles Zacharia Wambura (Mary Festo Bukumba). Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney
Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura na mkewe Mary Festo Bukumba wakiwa wamepanda pikipiki waliyopatiwa zawadi na Benki ya CRDB kwa kukimbiza sana miamala na kufungua akaunti nyingi. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana
Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura akitoa neno la shukrani baada kukabidhiwa pikipiki na Benki ya CRDB, kulia ni mkewe Mary Festo Bukumba. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Luther Mneney akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana
Mke wa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura bi. Mary Festo Bukumba akitoa neno la shukrani kwa benki ya CRDB
Wakala wa Benki ya CRDB Grace Joliga akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kwa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu na Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB, Mawakala wa Benki ya CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu na Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu na wafanyakazi wa Wakala wa Benki ya CRDB Charles Zacharia Wambura
No comments:
Post a Comment