BILLION 4.4 KUBORESHA HUDUMA ZA UCHUNGUZI MOI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, August 3, 2023

BILLION 4.4 KUBORESHA HUDUMA ZA UCHUNGUZI MOI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo (MOI), Prof. Abel Makubi akizungumza na waandishi wa Habari Leo Agosti 3,2023 Jijini Dodoma,wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo ndani ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya Sita na mipango ya Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Nsemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa,akizungumza na waandishi wa Habari Leo Agosti 3,2023 Jijini Dodoma,wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo ndani ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya Sita na mipango ya Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Waandishi wa Habari wakimfuatia ,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo (MOI), Prof. Abel Makubi, Leo Agosti 3,2023 Jijini Dodoma,wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo ndani ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya Sita na mipango ya Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Waandishi wa Habari wakimfuatia ,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo (MOI), Prof. Abel Makubi, Leo Agosti 3,2023 Jijini Dodoma,wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo ndani ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya Sita na mipango ya Mwaka wa Fedha 2023/2024.

Na Okuly Julius Dodoma

KATIKA jitihada za kuimarisha ubora wa huduma za uchunguzi katika Taasisi ya MOI, Serikali imetoa Tshs.Billion 4.4 kwa ajili ya ununuzi wa mashine mpya ya kisasa ya MRI na CT scan kwa lengo la kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma hiyo kwa uhakika na wakati bila ya kusubiri muda mrefu na kurahisisha ugunduzi wa magonjwa.


Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo (MOI), Prof. Abel Makubi wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hiyo ndani ya miaka miwili ya Serikali ya awamu ya Sita na mipango ya Mwaka wa Fedha 2023/2024.


Prof Makubi amesema lengo la kuimarisha huduma ni Kuongeza ubora wa huduma zote ndani ya MOI ili kukidhi matarajio ya Wananchi ndani ya nchi na kufikia viwango vya Kimataifa na kuvutia Utalii Tiba.


Aidha,Prof Makubi ametaja upasuaji wa kibingwa bobezi kuwa Jumla ya wagonjwa 14,574 walifanyiwa upasuaji ikilinganishwa na wagonjwa 13,618 waliofanyiwa katika 2019/2020 mpaka 2020/2021 ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.4%.


Sambamba na hayo Prof.Makubi amesema Katika Mipango ya utekelezaji wa Bajeti ya Fedha ya Mwaka 2023/24, Serikali imetenga jumla ya TZS 55.9 billion kwa MOI ili kuboresha huduma za Tiba na shughuli za uendeshaji.


Upasuaji mpya wa Kibobezi na zilizofufuliwa na kuimarishwa ambapo wagonjwa 31 wameondolewa uvimbe kwenye sakafu ya ubongo kupitia tundu la pua (transsphenoidal hypophysectomy), gharama za upasuaji huu hapa nchini ni Shilingi milioni 8 – 16 na nje ya nchi ni zaidi ya Shilingi milioni 40.


Prof.Makubi amesema kuwa tangu Mei 2023, wagonjwa 97 wamepata huduma ya kutibiwa maumivu sugu ya mgongo bila ya upasuaji, tangu Mei 2023. Gharama za upasuaji huu hapa nchini ni shilingi milioni 1 na nje ya nchi ni zaidi ya shilingi milioni 9.

Pia wamefufua huduma za Upasuaji Marudio ya vipandikizi (Revision Implant Surgery) ambapo wagonjwa 57 kwa kurekebisha nyonga na magoti kwa wagonjwa ambao walifanyiwa upasuaji kati ya miaka 15-19 iliyopita.




Kwa upande wake msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa amewataka watanzania kupata huduma za matibabu katika hospital na siyo kwenda kwa waganga wa kienyeji kwenda kutibiwa.


"Kutoa tiba za asili bila kibali kwanza ni kinyume Cha sheria na wengine wanawadanganya watu mpaka wanapoteza maisha kisa kuwaaminisha kuwa watawatibu Mimi nimepoteza ndugu zangu Kwa ajili ya hao waganga wa tiba za asili na ndio maana nawaambia watanzania nendeni hospitali mkapate huduma Kwa wataalamu,"amesema Msigwa


MOI, ilianzishwa na Serikali kwa Sheria ya Bunge Namba 7 ya mwaka 1996 Ikiwa na Majukumu ya Kutoa tiba za kibingwa kwa magonjwa ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya fahamu pamoja na kufundisha wataalamu na , kutoa ushauri na kufanya tafiti katika tiba za magonjwa ya mifupa na ubongo.

No comments:

Post a Comment