BMH YAJA NA SULUHU YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, August 1, 2023

BMH YAJA NA SULUHU YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME


Na Okuly Julius-Dodoma

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa (BMH) Dkt.Alphonce Chandika amesema Hospitali hiyo inaendelea kujivunia Huduma mbalimbali za Ubingwa Bobevu ambayo imekuwa ikitolewa katika HOSPITALI hiyo.


Dkt.Chandika ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa Habari Leo Agosti 1,2023 Jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji wa Shughuli mbalimbali na mwelekeo wa utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2023/24 katika Hospitali hiyo ya Benjamin Mkapa.


Katika nyanja ya Ubingwa Bobevu BMH imefanikisha Upandikizaji wa kipandikizi katika UUME Kwa Wananchi wawili ambapo Dkt.Chandika amekiri kumpokea matokeo mazuri kutoka Kwa Wananchi hao.


"Katika Mwaka wa fedha ulioisha tumetoa Huduma ya Upandikizaji wa kipandikizi kwenye Uume Kwa Wananchi 2 na nikiri tu mbele yenu waandishi wa Habari kuwa wale jamaa Kwa sasa wamerudisha Heshima kwenye familia wamekiri kuwa mambo ni safi,"amesema Dkt.Chandika


Pia amewataka wananchi wasione aibu kuja kupata huduma hiyo kwani si vyema kuendelea kukaa Kwa kusononeka wakati matibabu yanapatikana.


Dkt.Chandika amesema gharama za kupandikiza kipandikizi hicho kwenye Uume ni kuanzia milioni 6 mpaka 10 .


Ametoa wito Kwa Wananchi kuendelea kuzingatia Afya zao ili kuepukana na Magonjwa yanayopelekea kupoteza nguvu za Kiume ikiwemo kujikita katika ufanyaji wa Mazoezi na kula vyakula vyenye virutubisho stahiki.


VIPAUMBELE VILIVYOTEKELEZWA KWA MWAKA 2022/2023 KATIKA HOSPITALALI YA BENJAMIN MKAPA

  • upandikizaji figo, kwa mwaka wa fedha ulioisha jumla ya wananchi 8 wamenufaika na upandikizaji figo, wastani wa wahuduma hii ni shilingi 36,000,000 milioni ambapo kwa wanufaika 8 wametumia jumla ya shilingi 288,000,000 wakati hawa wangeenda nje ya nchi kupata huduma hii wangetumia shilingi 600,000,000/= kulingana na hospitali za nje, hivyo kwa huduma hii Serikali imeokoa shilingi 312,000,000.


  • Pili huduma za matibabu ya moyo, katika huduma hizi za moyo tumeendelea kuimarika kutoka mwaka hadi mwaka uliopita tumefanya uchunguzi wa Mishipa ya Moyo kwa wagonjwa 320, Upandikizaji Betri wagonjwa 13, Watoto waliozibwa Matundu kwenye Moyo 14, Kuweka vizibua njia ya Mishipa ya Moyo (Stents) 54.


  • Tatu huduma ya vipandikizi kwenye Magoti na Nyonga (Hip and total Knee Replacement) jumla ya wanufaika 72 wamenufaika na huduma hii. Serikali imetumia 864,000,000 milioni ambapo kama wangeenda kupata huduma hii nje ya nchi ingeigharimu Serikali shilingi 2,502,000,000/= bilioni.



  • Hivyo Serikali imeokoa shilingi 1,638,000,000/= Bilioni aidha katika matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi huduma ya Ubongo na Mishipa ya Fahamu wananchi wamenufaika na huduma hii kwa Upasuaji wa Ubongo 276 na Upasuaji Uti wa mgongo 237


  • Jambo la nne na kwa ukubwa ni huduma mpya iliyo zinduliwa mai 10 mwaka huu ni huduma ya upandikizaji uloto (Borne Marrow Tansplant) ambayo imeafanikiwa kwa manufaa makubwa kwa watoto wa nne wamepatiwa matibabu hayo na sasa wamepona kabisa.


  • Huduma hii inapatikana Tanzania pekee katika ukanda wa Afrika mashariki na Kati na ni Hospitali ya Benjamin Mkapa pekee inayotoa matibabu, gharama za matibabu ni shilingi 50,000,000/= wakati matibabu haya nje ya nchi yanapatikana kwa 120,000,000/= hadi 135,000,000/= Milioni hii ni kusema Serikali imedhamiria kuokoa pesa na kuimarisha huduma za matibabu Tanzania.


  • Jambo la tano la muhimu katika kiwango cha kufikia utoaji wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi nilazima mfanye mashirikiano ya kitaifa na kimataifa, katika hili niwe wazi Serikali ya Awamu ya Sita inayoongonzwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetufungulia na kutuwekea mazingira rafiki ya kufanya mashirikiano ya kimatibabu kama ifatavyo;
I. Help3 Monza ya nchini Italy
II. DKMS Laboratory ya nchini Ujerumani
III. Pathology without Bordarder – nchini Italy
IV. Shebba Medical Hospital – nchini Izrael
V. Childrens Heart Charity Association – nchini Kuwait
VI. Chuo kikuu cha Vienna&Hospitali kuu ya Vienna – nchini Austria
VII. Hospitali ya watoto Sanjeevani – nchini India


VIPAUMBELE KATIKA MWAKA WA FEDHA WA 2023/24

Ikumbukwe kuwa Hospitali ya Benjamin Mkapa inahudumia wananchi zaidi ya Milioni 10 wa mikoa ya Dodoma, Iringa, Singida, Manyara na baadhi ya maeneo ya mikoa ya Morogoro na Tabora.


Pia inapokea wananchi kutoka karibu kila kona ya nchi na nje ya mipaka ya Tanzania wanaokuja kufuata huduma za matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi, hivyo vipaumbele vilivyopo vimelenga kuifanya BMH kuwa Hospitali ya pili ya Taifa.



Kwa mwaka huu wa fedha tumetengewa shilingi 64,527,012,327/= Bilioni katika hizi shilingi 18,620,000,000/= Bilioni zinakwenda kwenye miradi ya maendeleo ili kuendelea kuwapunguzia wananchi adha ya kusafiri mbali kupata matibabu.


Pia Dkt.Chandika ametaja Maendeleo hayo kuwa ni kuendeleza ujenzi wa jengo la saratani ambao mpaka sasa umefikia asilimia 27, hivyo kwa kutengewa pesa hizi zitasogeza zaidi ujenzi.


Eneo lingine ni ujenzi wa jengo la matibabu ya moyo na kifua kwa watoto na watu wa zima(Cardiovascular and Thoracic Center) tunatarajia kuanza ujenzi huu mwaka huu wa fedha nayo ni katika lengo la kuwapunguzia adha wananchi kusafiri mbali kupata matibabu.


Pia ili kukabiliana na ongezeko la wagonjwa BMH kwa mwaka huu inatarajia kuongeza vyumba vya upasuaji ili kukidhi hitaji la wagonjwa.


Dkt.Chandika ameongeza kuwa katika Bajeti hiyo inakwenda kuwawezesha kujenga kituo cha Upandikizaji wa Figo (Kidney Transplant Complex) yenye vyumba vya upasuajia kwa anayechangia figo na anayepokea pamoja na ujenzi wa Maabara ya kuchukulia sampuli za wagonjwa, chumba cha wagonjwa mahututi, Famasia (duka la dawa), vyumba vya madaktari.



"Lengo la Serikali ambalo sisi tunalitekeleza ni kuhakikisha kuwa tunaondoa mwingiliano wa mgonjwa anayepandikizwa figo na wagonjwa wengine, tunamwondolea usumbufu kufuata huduma sehemu mbalimbali na kupunguza muda wa kusubili huduma kwa kuwa mgonjwa atahudumiwa sehemu moja na vile vile watoa huduma watapunguziwa usumbufu wa kutafuta kufuata vifaa kwenye idara nyingine,"


"Sote tunatambua kuwa Mheshiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amenunua mashine za X-Ray na Ultrasound karibu kila kituo cha Afya nchini, mashine hizo hutumika kufanya utambuzi wa aina ya ugonjwa na kiwango ambacho umefikia mapema ili kumwezesha mtoa huduma kuamua ikiwa tatizo hilo linaweza kutibika au kutolewa rufaa,"amesema Dkt.Chandika



No comments:

Post a Comment