Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella,akimkabidhi hati ya Kiwanja Mkurugenzi Mtendaji wa Counsenuth Bi.Shakila Mayumana, wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (CONSENUTH) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma.
Na. Gideon Gregory-CHEMBA
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Gerald Mongella amewahimiza wakazi wa kijiji cha Mrijo Juu wilayani Chemba mkoani Dodoma kuhakikisha wanatunza vyema kisima cha maji ambacho kimechimbwa kwa msaada wa kituo cha ushauri na saha lishe na afya (CONSENUTH) kwa kushirikiana na nchi ya Ireland.
Mhe.Mongela ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kisima hicho ambapo amesema adui mkubwa ni yule atakaye kwenda kuchezea chanzo cha maji na kuongeza kuwa tayari visima 12 vimeisha chimbwa huku vitano vikiwa vimesalia kufikia jumla 17.
Naye Mwakilishi wa Ubalozi wa Ireland Nancy Katalai amesema ubalozi wa nchi hiyo kwa muda mrefu umeelewa kuwa sababu za lishe duni na athari zake zinahusiana kwa karibu na sifa za kitamaduni ikiwemo kaya na jamii ambapo wanawake wanakosa mamlaka ya kufanya maamuzi ndani ya nyumba.
Awali akisoma risala ya mbele ya mgeni rasmi Mtendaji Kata ya Mrijo Juu Jesca Njiga amesema kisima hicho kimechimbwa na asasi ya Consenuth kwa ufadhiri wa Irish Aid kwa kushirikiana na serikali kupitia mradi wa lishe kijinsia.
“Kisima hiki kinauwezo wa kuzalisha lita 8000 kwa saa hivyo kitapunguza adha ya maji iliyokuwa ikiwakabili wananchi wetu kwa muda mrefu,”Amesema Njiga.
Njiga ameongeza kuwa kisima hicho hutumiwa na wafugaji kunyweshea mifugo yao, hivyo mradi huo utasaidia kuimarisha sekta ya ufugaji kijijini hapo.
Nao baadhi ya wanakijiji wa Mrijo Juu wakizungumza na Jambo FM wameipongeza CONSENUTH kwa juhudi zao katika kuhakikisha wanatatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji ambayo wamesema itawasaidi pia kubiliana na udumavu unaowakabili watoto.



Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella,akizungumza wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma
Mkurugenzi Mtendaji wa Counsenuth Bi.Shakila Mayumana,akitoa taarifa ya Mradi wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma
Mwakilishi wa Ubalozi wa Ireland Bi.Nancy Katalai,akizungumza wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma
Mtendaji wa Kata ya Mrijo Juu Bi.Jesca Njinga,akisoma risala wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella,akizindua mradi wa Maji unaosimamiwa na Counsenuth wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella,akimtishwa Ndoo ya Maji Mwananchi mara baada ya kuzindua mradi wa Maji unaosimamiwa na Counsenuth wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella,akimkabidhi hati ya Kiwanja Mkurugenzi Mtendaji wa Counsenuth Bi.Shakila Mayumana, wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella,akiwakabidhi zawadi washindi wa michezo mbalimbali wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella,akiwa katika picha mbalimbali wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment