Waziri Kijaji ameyasema hayo Agosti 3, 2023 alipotembea Kiwanda cha kuzalisha Maziwa cha Tanga Fresh kilichopo jijini Tanga kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji wa maziwa na kusikiliza na kutatua changamoto walizonazo.
Aidha amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inafanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha wafanyabiashara na wawekezaji wanakuwa na mazingira bora na wezeshi ili kufanya biashara kwa tija na kukuza uchumi wa Taifa.
Vilevile amesema Serikali ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Tanzania inataka kuona wafugaji wanabadilika kutoka katika ufugaji wa kienyeji kwenda katika uwekezaji wa kisasa ili kukidhi mahitaji ya soko.
Aidha amepongeza kiwanda hicho kwa ajira walizotoa hapa nchini na ametaka ajira zisiso za moja kwa moja ziongezeke.
No comments:
Post a Comment