SERIKALI KUKIWEZESHA KIWANDA CHA KMTC KUFIKIA MALENGO YAKE- DKT.KIJAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, August 4, 2023

SERIKALI KUKIWEZESHA KIWANDA CHA KMTC KUFIKIA MALENGO YAKE- DKT.KIJAJI


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Serikali itahakikisha inakisaidia Kiwanda cha kutengeneza Vipuri Kilimanjaro ( KMTC) kufikia malengo katika masoko kwa kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuona uzalishaji wa ndani unafanyika kupitia chuma kinachozalishwa nchini.


Amesema hayo Agosti 2, 2023 alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Kilimanjaro kujionea shughuli zilizopo pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto zao.


Aidha amewapongeza wafanyakazi wa kiwanda hicho na kuwataka kuwa waaminifu kwa kuwa Serikali inafanya jitihada mbalimbali za kuweka mazingira bora ya biashara ili kuvutia wawekezaji katika viwanda vitakavyotumia vipuri vinavyotengenezwa na kiwanda hicho.

No comments:

Post a Comment