KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAJI NA MAZINGIRA YAKUTANA NA WIZARA YA MAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, August 15, 2023

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAJI NA MAZINGIRA YAKUTANA NA WIZARA YA MAJI


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira leo imekutana na Wizara ya Maji na kupata taarifa ya Sekta ya Maji na mwenendo wake hapa nchini.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiongoza Sekta ya Maji na watendaji wake katika kikao hicho cha kamati amesema upatikanaji wa maji mwezi Julai 2022 hadi Juni 2023 kwa mjini umepanda kwa wastani wa asilimia 88 na unatarajiwa kufika asilimia 91 mwezi Desemba 2023. Kwa upande wa vijijini amesema hali ya huduma imeongezeka kutoka asilimia 77 na inatarajiwa kufika asilimia 80 mwezi Desemba 2023.

Waziri Aweso amesema nia ni kufika lengo la asilimia 95 mjini na asilimia 85 vijijini, na Sekta ya Maji ipo tayari kwa maoni na ushauri wa Kamati ya Maji na Mazingira ili kufanikisha lengo hilo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Jackson Kiswaga (Mb) ametumia kikao hicho kuipongeza Sekta ya Maji kwa kazi kubwa inayofanyika katika miradi ya maji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma endelevu, na kuleta mabadiliko katika jamii.



No comments:

Post a Comment