Na OR TAMISEMI
Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Subisya kabuje amesema Serikali imedhamiria kusogeza huduma za Ustawi kwa Jamii kwa Wananchi hasa wale waliopo katika mazingira hatarishi na wanaokuMbwa na changamoto za kijamii.
Bi. Kabuje ameyasema hayo kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI katika halfa ya Uzinduzi wa Madawati ya huduma za Ustawi wa Jamii katika vituo vya usafirishaji Nchini na uzinduzi wa Kiongozo cha Taratibu na Utoaji wa Huduma za Ustawi wa Jamii Kwa Watoto wanaoishi na kufanya Kazi mitaani iliyofanyika katika stendi ya Magufuli Jijini Dar es Salaam.
“Dawati hili ni kielelezo cha utayari wa Serikali kusogeza huduma za kijamii karibu zaidi na wananchi hasa wale walio katika mazingira hatarishi kama Watoto waliopotea ama kutoroka familia zao, Watoto ambayo ni wahanga wa biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu na wahanga wa vitengo vya kikatili na kijinsia waliopo safarini” alisema Bi. Kabuje.
Amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI Kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaendelea kusimamia madawati hayo na kuhakikisha yanaungwa mkono katika Halmashauri zote.
Naye, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dorothy Gwajima amewataka Wazazi na Walezi kutekeleza wajibu na majukumu yao kwani Serikali imeweka Mifumo mbalimbali ili kupambana na changamoto ya Watoto wa wanaoishi mazingira hatarishi.
“Serikali imeweka Mifumo mbalimbali ya kusababisha Jambo hili lisitokee lakini Jambo hili linatokea kwasababu baadhi ya Wazazi na Walezi hawatimizi wajibu wao kikamilifu katika malezi ya Watoto” alisema Mhe. Gwajima.
Amesema Kiongozo hicho ambacho kimezinduliwa kitasaidia katika kuongoza kwenye huduma za vituo vya usafirishaji na kubaini mapema viashiria vya hatari vya ukatili.
Madawati haya ya huduma za Ustawi wa Jamii katika vituo vya usafirishaji yamezinduliwa katika Mikoa 11 nchini ambapo hadi sasa kuna jumla ya madawati 14 ambayo wanawezeshwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Railway Children Africa.
No comments:
Post a Comment