Na Okuly Julius-Dodoma
Dkt.Gwajima ameyasema hayo Leo Agosti 30,2023 Jijini Dodoma,wakati akifungua Mkutano wa robo mwaka wa Wadau wa Ustawi wa Jamii.
Amesema Vitendo hivyo vinaweza kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo madhara kimwili, kafya, kisaikolojia na kiuchumi na kuongeza kuwa Vitendo hivyo pia vimeendelea kutokea katika nchi zote duniani zilizoendelea na zinazoendelea ikiwemo Tanzania ambapo vinasababisha madhara makubwa kwa mtu binafsi, familia, jamii na Taifa kwa ujumla.
Aidha,Vitendo vya ukatili vinaathiri ukuaji wa watoto na vinasababisha nguvu kazi dhaifu isiyokuwa na tija ya kutosha katika Taifa kwa siku za usoni.
“Sisi sote tumekuwa tukisikia matukio mbalimbali ya watu kudhuru wengine au wao wenyewe kujidhuru kutokana na msongo wa mawazo, Hivi karibuni kumetokea tukio la kusikitisha mkoani Arusha kuhusu mama kujinyonga kwa kushindwa kurejesha mkopo. Hivyo, niwaombe wadau na maafisa Ustawi wa Jamii tubuni njia mbadala ya kuwasaidia na kutoa elimu kwa wanawake wanaojiingiza kwenye shughuli za maendeleo ya kiuchumi zinazohusisha mikopo mbalimbali ili kuwaepusha na madhara makubwa yanayopelekea hadi wengine kupoteza uhai na kuacha familia katika mazingira hatarishi,”amesema Dkt. Gwajima.
Hata hivyo amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwa mila na desturi potofu zinazopelekea ukatili katika jamii, serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kukabiliana na hizo ni Kuanzishwa kwa Mfumo Jumuishi wa Kitaifa wa Kushughulikia Mashauri ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi nchini.
Pia Kuundwa kwa kamati ya Kitaifa inayotekeleza afua za kushughulikia tatizo la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.
Kwa upande wa Wadau wa Ustawi wa Jamii nchini Tanzania wameishauri serikali kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali zakuwalinda Watoto na wahanga wa vitendo vya ukatili ikiwemo sheria ya adhabu ya makosa ya mtandao na sheria ya Ushahidi kwa Watoto.
Ambapo wamejadili afua za kupinga vitendo hivyo kwenye jamii ambapo wamebainisha kuwa bado kundi la Watoto ndio linakumbwa sana na vendo vya kikatili hivyo lazima hatua za haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya Watoto.
Waliongeza kuwa “Wizara inaendelea na mchakato wa kuweka mabadiliko ya sheria mbalimbali ili kuhakikisha mtoto analindwa katika maeneo yote ndani ya mtandao na nje ya mtandao, kama unavyojua kutokana na maendeleo ya sasa ya teknolojia ambayo watoto wanatumia mitandao hivyo kuna uhitaji kutunga sheria ili tuweze kuwalinda watoto kwenye mitandao kwani sheria ya mtoto wa sasa imemlinda mtoto kwa kumzuia kwenye sherehe za usiku, lakini kama unavyojua sasa watoto wanaweza kuwa mtandaoni nawasiliana na mtu kupitia mtandao lakini ukiangalia kwasheria ya sasa haijamlinda mtoto katika mazingira hayo na sisi wadau tumeona sasa kama kuna haja ya kuongeza wigo wa ulinzi wa mtoto katika mtandao kwa kuhakikisha tunapiga marufuku kwa watu wazima au mtu yeyote atakayeweza kufanya” walisema wanapinga vurugu.
“Hivyo tunashauri Sheria ya Adhabu ya makosa ya mtandao ibadilishwe ili kuongeza wigo wa ulinzi kwa watoto mtandaoni, kwani tatizo hilo linachukuliwa kuwa kubwa baada ya tafiti ndogo naona sioni kuwa watoto wengi wanapigiwa simu na kujihusisha na mitandao kwa sababu ya ukweli kwamba watoto wengi wanapigiwa simu na kujihusisha na mitandao, hata sisi wazazi tunatoa simu kwa watoto kucheza michezo ya mtandaoni lakini unaweza kukuta mtoto badala ya kucheza mchezo alioutaka anafanya mambo mengine yasiyo ya kimaadili nakutana na watu wapo mtandaoni nakuanza kuwasiliana nao kwa njia zisizosahihi.
“Lakini tunashauri marekebisho ya sheria nyingine yagawanywe na kurekebisha sheria ya ushahidi kwa watoto kwani kwa sasa sheria inamtaka mtoto akisikilizwa mahakama inahakikisha mtoto anakuwa na uwezo wa kuelewa kuwa anawajibika kusema ukweli lakini sasa unakuta mahakama inasikiliza wakati mwingine unakuta haijaandika utaratibu uliotumia kuhakikisha mtoto anajua umuhimuwalisema ukweli, sasa kesi inaweza kuonekana kuwa hakuna uhakika kwakua hakuna vyeti inaleta shaka kwa mtoto na inaweza kutumika kama kukata rufaa kukua ataonekana mtoto ushahidi wake hauna uhakika na hiyo inatoa faida kwa mtuhumiwa ambaye anaweza kuwa ametendamakosa dhidi ya watoto"walisema wadau wanaopinga vitendo vya ukatili.
“Tunashirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria na tumeshawasilisha pendekezo letu la kurekebisha sheria ya ushahidi ili iweke utaratibu mahususi ambao mahakama italazimika kuhakikisha zinarekodiwa kwa lazima na mahakama zinazorekodi utaratibu kuhakikisha mtoto anajua umuhimu wa kusema ukweli
“Walisema changamoto kubwa bado ipo katika ukatili wa kisaikolojia na wengi wanaofanya vitendo hivyo wanatokea kwenye familia hasa wazazi na walezi wakiwa hawajajitambua wamekua wakilinganisha watoto wao na matukio ambayo kwa kiasi fulani walikua wamewatendea watoto ukatili bila wao kujua kama wanatenda ukatili.”
“Mzazi anaweza kutoka na watoto wake kwenda sehemu nzuri ambayo yeye kwa umri wake ni sahihi wanafurahia lakini katika mazingira yale unaweza kukuta anamuweka mtoto wake kwenye vitendo ambavyo mwisho wa siku vinamfanyia ukatili wakisaikolojia , lakini pia kukingana na maendeleo ya tekinolojia tumekua watumiaji wakubwa sana wa taarifa kupitia mitandao ya kijamii , sasa ukiingia kwenye mitandao ya kijamii utakuta matukio mengi yanaripotiwa wengine wanaripoti kama sehemu yakuonyesha uwezo wao wakuwahudumia watoto, lakini wengine pia wanakuta wanachangamoto za kimaisha wanatafuta usaidizi kwaajili ya watoto hao , lakini katika kutafuta huduma au kuonyezha uwezo bado matukio mengine hayohayo yanasababisha mtoto unaweza kukuta kwa mfano mzazi anarekodiwa wakiwa wanacheza mtindo ambao kiasi fulani haina tija kwenye makuzi na maendelelo yao hivyo vitendo hivyo havina afya kwa makuzi ya mtoto na mwisho wa siku kuna kua na vizazi visivyo na maadili”.
No comments:
Post a Comment