ACP. MBAO AWATAKA MADEREVA BODABODA KUTOKUBALI KUTUMIKA KUFANYA UHALIFU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 26, 2023

ACP. MBAO AWATAKA MADEREVA BODABODA KUTOKUBALI KUTUMIKA KUFANYA UHALIFU


Na Mwandishi wetu -Dodoma 

Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi Acp. Boniphace Mbao awataka waendesha bodaboda kuzingatia Sheria za usalama barabarani kwa kujali watumiaji wengine wa ili kuendelea kubaki kuwa salama na kupunguza ajali kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kitendo Cha usalama barabarani

Ameyasema hayo Leo Septemba 26,2027 wakati akizungumza na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda katika eneo la majengo Sokoni.


Aidha Acp Mbao amewakumbusha waendesha bodoboda kuwa na leseni kwani ndio kitu muhimu kinachowaruhusu kuingia katika barabara za umma na nilazima wahakikishe pikipiki iwe imekatiwa bima ili ikitokea bahati mbaya imetokea ajali pikipiki imeharibika waweze kupata fidia na abiria aliye mbeba kupitia shirika ambalo wamekatia bima


"Hata hivyo Acp Mbao amewasisitiza madereva hao kuvaa kofia ngumu na abiria wanaowabeba kwasababu kofia ngumu itakusaidia ikiwa imetokea ajali kutopata madhara makubwa kwasababu tunaamini kichwa hiki alichotuumbanacho Mungu hakina spea ndo Maana serikali iliona busara bodaboda mnaofanya biashara ya usafirishaji kwa kutumia pikipiki ni lazima uendeshe ukiwa umevaa kofia ngumu," amesema ACP Mbao

Amesema kuna mambo yakuzingatia unapotumia barabara huruhusiwi kupakia abiria zaidi ya mmoja haya ni maelekezo ya Sheria lengo ni usalama wetu Kwanza pia usiende mwendo Kasi unapoendesha pikipiki lazima uzingatie ukomo wa spidi kwa kuzingatia vibao vilivyowekwa barabarani kwenye makazi ya watu usiende mwendo Kasi na usitumie kileo chochote ili uendeshe pikipiki na umfikishe abiria salama


Aidha Acp Mbao amewakumbusha waendesha bodaboda juu ya utumiaji wa zebra eneo ambalo limekuwa ni tatizo kwa bodaboda na kumekuwa na ajali nyingi zikitokea kwa kutokufuata sheria na alama za barabarani uzembe mdogo wa mtu unasababisha madhara makubwa kwa wengine lazima kwenye zebra usimame ili tuendelee kuleta usalama katika maeneo yetu.

Acp Mbao amewata kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu na kuacha kutumika kuwabeba wahalifu kwasababu ukimbeba mhalifu kwenda kufanya uhalifu wowote au uvunjaji unakuwa mshiriki wa kosa kwa mujibu wa sheria

Sambamba na hilo Acp Mbao amewata waache Mara moja kujichukulia sheria mkononi mfano ajali inapotokea kwa bahati mbaya kumekuwa na tabia za kumpiga mtu huo sio ubinadamu na sheria haitaki hivyo kinachotakiwa ni kutoa taarifa kwa Jeshi la polisi ili tuweze kumshughulikia yule mtu kwa mujibu wa sheria na kumekuwepo na bodaboda wakigongana wanaondoa vielelezo wengine wanatorosha pikipiki utaratibu ni lazima zifikishwe kituo Cha polisi kwa hatua zaidi na sio kufanya kinyume Cha sheria.

No comments:

Post a Comment