DKT. CHANA KUTATUA TATIZO LA UFINYU WA BAJETI THBUB. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 7, 2023

DKT. CHANA KUTATUA TATIZO LA UFINYU WA BAJETI THBUB.


Na. Gideon Gregory Dodoma.

Waziri wa katiba na sheria balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa wizara itaenda kulifanyia kazi tatizo la bajeti linaloikabili Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), ili iweze kutekeleza vyema majukumu yake.

Dkt. Chana ametoa kauli hiyo leo Septemba 7,2023 wakati wa ziara yake katika ofisi za tume hiyo ambapo amesema tayari wao kama wizara wameshaanza kuweka mikakati ya namna watakavyokuwa na bajeti ya kutosha.


“Lakini kule wizarani tunaweza kupata washirika ambao ukifanya nao kazi hawaingilii mipaka yako ya nchi, kwahiyo hilo ni eneo ambalo tunaweza tukashirikiana nao kwa namna moja ama nyingine hatupendi washirika watakao tupa masharti lakini mnashirikiana katika kuleta maendeleo,”amesema Dkt. Chana.

Amesema lazima tume iwe na ofisi za kanda za uhakika maana hiyo ni tume hiyo ipo ndani ya kikatiba pamoja na kuendelea kutafakali bajeti ya masuala ya maendeleo.


Kwa upande wake Naibu Waziri Mhe. Pauline Gekul amesema wizara hiyo ina jumla ya taasisi 10 ambapo THBUB ndiyo yenye bajeti ndogo.

“Mhe. Waziri kupitia wewe tunaamini na sisi wasaidizi wako jambo hili tutaendelea kulisukuma kwakuwa tumepewa Bilioni 1.6 kwenye bajeti ya sasa nadhani tutaendelea kuwapigania kwani kazi yao ni kubwa sana,”amesema Gekul.

Akiwasilisha taarifa ya tume hiyo MwenyekitiJaji mstaafu Mathew Mwaimu amesema kuwa pamoja na kazi wanazozifanya wanakabiliwa na ufinyu wa bajeti.

Amesema tume inapata fedha pungufu za matumizi mengineyo ikilinganishwa na bajeti inayoidhinishwa ambapo kwa mwaka 2022/23 ilipokea 78% hali iliyoikwamisha THBUB kufikia malengo ya utekelezaji kwa mwaka husika.


“Kama nilivyotangulia kusema changamoto nyingine ya tume inayoidhinishwa kuwa ndogo ikilinganishwa na mahitaji ya tume, kwa mfano kwa mwaka huu wa fedha 2023/24 tume ilihitaji kiasi cha Bilioni 9 kwaajili ya matumizi mengineyo lakini kiasi kilichoidhinishwa ni zaidi ya Bilioni 5,”amesema Jaji Mwaimu.

Aidha, amemuomba Waziri kuendelea kuipigania THBUB ili iweze kuongezewa bajeti ya kuwezesha kutekeleza majukumu yake kama ilivyopendekezwa na tume ya haki jinai na kuwafikia wananchi wengi kwa wakati hasa wale wa vijijini na makundi maalum kama vile wanawake, watoto na wenye ulemavu.

No comments:

Post a Comment