DKT.BITEKO AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI KAGERA ,,,,,,AWASHA UMEME KIJIJI CHA MUBABA NA NYANTAKARA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, September 27, 2023

DKT.BITEKO AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI KAGERA ,,,,,,AWASHA UMEME KIJIJI CHA MUBABA NA NYANTAKARA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko, (wa Nne
kutoka kulia) akikata utepe kuashiria umeme kuwashwa katika Kijiji cha
Mubaba wilayani Biharamulo mkoani Kagera. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa
wa Kagera, Fatma Mwasa.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko, (wa Nne
kutoka kulia) akikata utepe kuashiria umeme kuwashwa katika Kijiji cha
Mubaba wilayani Biharamulo mkoani Kagera. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa
wa Kagera, Fatma Mwasa.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko, (wa Pili
kutoka kulia) akiwasha umeme katika moja ya nyumba katika Kijiji cha
Nyantakara wilayani Biharamulo mkoani Kagera ikiwa ni ishara ya
kuwasha umeme kwenye Kijiji hicho.

Teresia Mhagama na Godfrey Lulinga

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko, leo ameanza
ziara ya kikazi katika Mkoa wa Kagera ambapo katika siku ya kwanza ya
ziara yake amewasha umeme katika Kijiji cha Mubaba na Nyantakara
vilivyopo wilayani Biharamulo.

Akizungumza na wananchi pamoja na viongozi wa Serikali na wakandarasi
wa umeme vijijini, Dkt.Biteko ameagiza kuwa, sehemu zinazotoa huduma
za kijamii kama vile shule, visima vya maji na vituo vya afya zipewe
kipaumbele katika kupelekewa umeme ili wananchi waweze kupata huduma
bora.

" Haileti maana umeme kufika katika eneo fulani kama watoto wanasoma
gizani, haileti maana umeme kufika hapa halafu kina mama
wanajifungulia gizani, wala haina maana umeme kufika hapa wakati kuna
vyanzo vya maji na tunashindwa kuwapelekea maji watu wetu, ndio mana
Rais wetu anataka mfikiwe na umeme ili usaidie kuboresha huduma na
kuchagiza shughuli za uchumi ." Amesema Dkt.Biteko

Dkt.Biteko ametoa wito kwa wananchi kulinda miundombinu ya umeme na
wawakemee watu wanaoiba miundombinu ya umeme ikiwemo nguzo, mafuta ya
transfoma kwani wanarudisha nyuma jitihada za kuwafikishia umeme wa
uhakika wananchi.

Kuhusu wakandarasi wanaosimamia miradi ya umeme amesema kuwa,
wahakikishe wanafanya kazi kadri ya mikataba inavyoelekeza na kwamba
kama kuna changamoto zozote wazieleze kwa viongozi, lakini REA wakiona
kuna mkandarasi ambaye hafanyi kazi kama inavyotakiwa, mkandarasi huyo
aondolewe na awekwe mwenye uwezo.

Katika hatua nyingine, Dkt.Biteko amesema kuwa atasilimamia ipasavyo
agizo la Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan la kudhibiti changamoto ya
kukatika mara kwa mara kwa umeme ndani ya kipindi cha miezi sita.

" Agizo hili la Mhe.Rais tutalisimamia na kuhakikisha shida hii
tunayoiona ndani ya kipindi cha miezi tunaipunguza kwa kiasi kikubwa
ili watanzania wapate umeme wa uhakika."Amesema Biteko

Kuhusu nishati safi ya kupikia amesema kuwa, Serikali inakuja na
mpango utakaowezesha wananchi kupunguza matumizi ya kuni na mkaa wa
asili ambao una athari kwa afya na kuleta nishati safi ambapo REA
inakuja na mpango unaojumuisha kugawa mitungi ya gesi kwa wananchi
kwani lengo la Serikali ni kuhama kutoka nishati isiyo safi na kwenda
kwenye nishati safi.

No comments:

Post a Comment