DKT.JAFO AWAONYA WANAOSAFIRISHA TAKA HATARISHI NJE YA NCHI BILA VIBALI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, September 22, 2023

DKT.JAFO AWAONYA WANAOSAFIRISHA TAKA HATARISHI NJE YA NCHI BILA VIBALI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais , Muungano na Mazingira, Dkt.Selemani Jafo, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu ukiukwaji wa matakwa ya sheria ya usimamizi wa Mazingira na kanuni zake wakati wa kusafirisha nje ya nchi aina mbalimbali ya Chuma chakavu,Leo Septemba 22,2023 Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais , Muungano na Mazingira, Dkt.Selemani Jafo, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu ukiukwaji wa matakwa ya sheria ya usimamizi wa Mazingira na kanuni zake wakati wa kusafirisha nje ya nchi aina mbalimbali ya Chuma chakavu,Leo Septemba 22,2023 Jijini Dodoma.

Na Okuly Julius-Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais , Muungano na Mazingira, Dkt.Selemani Jafo amesema kupitia usafirishaji wa taka hatarishi nje ya nchi bila kibali husababisha Serikali kukosa mapato yanayopaswa kulipwa kupitia usafirishaji huo.

Dkt.Jafo ametoa kauli hiyo Leo Septemba 22,2023 Jijini Dodoma ,wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu ukiukwaji wa matakwa ya sheria ya usimamizi wa Mazingira na kanuni zake wakati wa kusafirisha nje ya nchi aina mbalimbali ya Chuma chakavu.

"Zipo tozo ,ada na Kodi zinazopaswa kulipwa kwa ajili ya kusafirisha taka ama Chuma chakavu nje ya nchi na tozo hizo zimewekwa na Serikali kupitia TRA kwa mujibu wa sheria kwa hivyo kitendo Cha utoroshaji wa aina yeyote unaikosesha Serikali mapato,"

Na kuongeza kuwa"utoroshaji huo pia unaweza kusababisha uharibifu wa miundombinu kutokana na kutofuatwa kwa sheria na Miongozo ya Serikali iliyopo na suala la usafirishaji wa aina yeyote ya Chuma chakavu nje ya nchi bila kuwa na vibali ni uvunjaji wa sheria za nchi,"amesema Dkt.Jafo

Dkt.Jafo ameongeza kuwa,katika kipindi Cha Mwezi Machi hadi Septemba, 2023, Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Waziri mwenye Dhamana ya Mazingira,haijatoa kibali Cha kusafirisha Chuma dongo nje ya nchi, huku kukiwa na taarifa ya usafirishaji wa Chuma chakavu na Chuma dongo katika kipindi hicho jambo ambalo ni kinyume Cha Sheria.

"Kuna baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu ambao wanakiuka matakwa ya sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura ya 191 na kanuni zake kwa kusafirisha nje ya nchi Chuma chakavu vya aina mbalimbali vikiwemo Chuma dongo bila kuwa na vibali vinavyotolewa na Waziri mwenye Dhamana ya Mazingira,"

Na kuongeza kuwa"tahadhari inatolewa kwa yeyote anayejishughulisha na Shughuli za kukusanya, kuhifadhi, kusafirisha ndani ya nchi, kuingiza nchini, kusafirisha nje ya nchi na kupitisha nchini taka hatarishi bila kibali ,atakuwa ametenda kosa la kisheria na atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria,"ameeleza

Amesema ,Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo Mkubwa katika suala la uwekezaji wa viwanda vya ndani kwa lengo la kuzalisha ajira na kukuza uchumi,hivyo usafirishaji wa bidhaa mbalimbali za Chuma chakavu ikiwemo Chuma dongo (caste Iron) nje ya nchi kiholela na usiofuata utaratibu unaweza kusababisha upungufu wa malighafi kwenye viwanda vinavyotumia malighafi za aina hiyo hapa Nchini.

Aidha,Dkt. Jafo amezielekeza Mamlaka za udhibiti zilizopo kwenye maeneo ya mipaka mbalimbali nchini kuhakikisha kwamba shehena yoyote ya taka hatarishi ikiwemo Chuma dongo inayosafirishwa nje ya nchi,inafuata masharti ya Kanuni za Udhibiti na Usimamizi wa Taka Hatarishi za Mwaka , 2021 ikiwemo kuwa na kibali kilichoyolewa na Waziri mwenye Dhamana ya Mazingira.

No comments:

Post a Comment