MSIACHE KUTUMIA DAWA ZA KUFUBAZA VVU -MAJALIWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 7, 2023

MSIACHE KUTUMIA DAWA ZA KUFUBAZA VVU -MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kilele cha Mdahalo wa Kitaifa wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virus vya Ukimwi ( NACOPHA) jijini Dodoma, Septemba 7, 2023.

Na Okuly Julius-Dodoma

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi wote waliopima virusi wakabainika kuwa wana virusi vya Ukimwi wakatumia dawa za kufubaza na wakajiona wamepona wasiache kutumia dawa hizo ghafla.


Waziri Mkuu Majaliwa alizungumza hayo Jijini Dodoma Leo Septemba 7,2023,wakati wa Kuzindua Mpango Mkakati wa 4 wa NACOPHA (2023-2028) iliyokwenda sambamba na Kilele cha Mdahalo wa Kitaifa wa Baraza la Taifa la Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA).


Waziri Mkuu amesema kwa wale waliokuwa wakitumia dawa wakapima mara moja, mbili au tatu wakajiona wamepona wasiache ghafla kutumia dawa kwani wataalamu wanasema mtu huyo akiacha matumizi ghafla anaweza kupata athari.


"Waliokuwa wameathirika wakatumia dawa za kufubaza wakarudia kupima mara tatu wakajiona wamepona, wasiache kutumia dawa ghafla hadi itakaposemwa vinginevyo, amesema Majaliwa



Waziri Mkuu amewataka kuzingatia ushauri wa wataaamu msiache ghafla hadi madaktari watakaposema vinginevyo.


Waziri Mkuu amempongeza Mwenyekiti wa NACOPHA Leticia Morice kwa baraza hilo kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake 2003 kwani katika kipindi cha muda huo amefanya jitihada kubwa katika kudhibiti Ukimwi nchini kwa kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali.


"Watendaji wote wa serikali na kwenye taasisi wekeni mpango kazi wa utekelezaji wa maazimio hayo ili katika mkutano ujao mpime matokeo ya mkutano huu wa mwaka huu.


Wadau wote wa maendeleo waendelee kushirikiana na baraza la NACOPHA na wadau wengine kuweka mkakati wa pamoja na kutimiza kuiwezesha Tanzania kutumia fursa mbalimbali kufikia malengo yaliyowekwa.


Serikali, wadau wa maendeleo sekta binafsi wanatakiwa waunganishe nguvu kufanya uwekezaji unaohitajika ili kuweka mazingira ya uwepo wa huduma bora za kutokomeza Ukimwi kuwa endelevu.


Wote waliohudhuria katika mdahalo ni vema kutambua kwamba wana jukumu kubwala kuhuisha mipango, Sera na ahadi zenu,mipango na kuwezesha nchi kufikia malengo ya kutokomeza Ukimwi nchini.


Pia waziri Mkuu amewataka wadau, NACOPHA na serikali kuendelea kushirikiana katika kampeni ya kutokomeza Ukimwi na kufikia malengo ya zero tatu ifikapo 2030.



"Kutokana na mkakati huo nchi imevuka lengo la 2025 kwani kwa sasa asilimia 96 wanajua hali zao, leo hii asilimia 98 wanaojua hali zao wapo kwenye ARV na asilimia 97 wanafubaza wingi wa virusi kwenye damu.


Serikali imehakikisha huduma, dawa na mafunzo kwa wananchi zinafikishwa, tunahitaji watu wakapime baada ya kurekebisha sheria kila mtu akapime.


Amewapongeza NACOPHA kwa kazi nzuri ya kuhamasisha jamii, vijana kufanya urakibishi, wanaume kujitokeza kupima na akatoa rai kuendeleza ushirikiano huo katika kampeni hiyo.


Pia ameipongeza NACOPHA kwamba wametoa mchango mkubwa wa kuimarisha mwitikio katika jamii kujitokeza kupima ili kujitambua hali zao, kupiga vita unyanyapaa, mmetoa elimu na hamasa ya kutumia huduma za ukimwi.



"Mmefanya utetezi wa uradhabishaji na kuongeza ushiriki wa vijana kupima, kutoa huduma ya maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa watoto na kuhamasisha wanaume kupima na kupika vita ukatili wa kijinsia," amesema.


Pia amepongeza usimamizi mzuri wa kampeni ya kutokomeza Ukimwi kwa uwepo wa NACOPHA na uwepo wa konga katika halmashauri mbalimbali nchini umesaidia kupunguza maambukizi mapya na mkakati ni kufikia zero tatu ifikapo 2030.


Bado matendo ya kunyanyapaa na ubaguzi katika jamii yanaendelea akawataka wadau kwa ujumla wao waendelee kutoa elimu shuleni, ofisini na kuandaa vitendea kazi ili kuwafikia wanafunzi wa vyuo vikuu, sekondari kuanzisha vilabu, masomo na kupunguza kwa kasi vya sekondari.



Amewapongeza wadau kufanikisha wakuu wa mikoa Dar es Salaama kuhamasisha watu kuchangia kuhamasisha ufanikishaji wa mtandao kufanya mdahalo na mkuu wa mko wa Dodoma kufanikisha mdahalo huu.


Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Mhe.Jenista Mhagama amewataka Wanaume kuacha tabia ya kutumia wake zao kama vipimo kwani wanaume walio wengi wanawatuma wake zao wakapime ndio watumie vipimo vile.


"Wanaume wengi siku hizi hawapimi VVU wanawatuma wake wao wakapime alafu wao ndio wanachukua vipimo vile na kutamba navyo mtaani,"amesema Mhagama.


Naye Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoshi na VVU (NACOPHA) Bi.Leticia Mourice ameishukuru Serikali,Wabia na Wadau mbalimbali Kwa kuendelea kuwawezesha watu wanaoishi na VVU kupata dawa na huduma zingine.


"Zamani tulikuwa tunaishi Kwa matumaini na Watu wengine walikuwa wanatuambia sisi ndio washika funguo za Nyumba za kuhifadhia maiti ila Kwa sasa tunaishi Kwa uhakika na maisha yamekuwa ya uhakika kutokana na kupata huduma stahiki ikiwepo dawa za kufubaza VVU ," amesema Bi.Leticia



No comments:

Post a Comment