‘NAIREJESHA TAMISEMI KWA WANANCHI’ MHE. MCHENGERWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, September 4, 2023

‘NAIREJESHA TAMISEMI KWA WANANCHI’ MHE. MCHENGERWA


OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema atairejesha wizara hiyo kwa wananchi kwa kuhakikisha viongozi wote wanasikiliza na kutatua kero zao kwa wakati.

Pia amewaonya watendaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambao ni wabadhilifu, wala rushwa na wasiowajibika katika utendaji kazi wao hawatakuwa sehemu ya utendaji kazi wake.

Mchengerwa ameyasema hayo leo Septemba 4, 2023 Jijini Dodoma mara baada ya kuwasili katika Ofisi za TAMISEMI zilizopo Mji wa Serikali, Mtumba.


“Niwaombe watumishi wenzangu kuwa sasa tunairejesha Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa wananchi, maana yake tunataka kufanyakazi hasa ili tuweze kufanikiwa na malengo ya Mheshimiwa Rais yaweze kutimia, hivyo lazima tufanyekazi usiku na mchana hakuna namna. Wizara yetu tunaisogeza kwa wananchi, tutasikiliza kero za wananchi.”amesema

Mchengerwa ametumia fursa hiyo kuwaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanatoka ofisini na kwenda kusikiliza na kutatua kero za wananchi na kusisitiza kuwa asilimia 45 ya wakuu wa wilaya hawafanyi majukumu yao.


“Kuanzia sasa wakuu wa mikoa wote, wakuu wa wilaya washuke chini kusikiliza kero za wananchi, asilimia 45 ya wakuu wa wilaya hawafanyikazi kabisa, hawasikilizi kero za wananchi, kwa hiyo tunataka kila mmoja afanyekazi ili tuweze kutimiza malengo ya watanzania, malengo ya Chama cha Mapinduzi, malengo ya Rais wetu.”

Kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Mchengerwa amewaonya wakurugenzi wa halmashauri ambao wamekalia fedha za miradi na kusisitiza kuwa hataongeza muda wa utekelezaji wa miradi hiyo.

“Mheshimiwa waziri (Kairuki) umesema kuna miradi mingi ambayo tayari imeshaanzwa lakini kuna baadhi ya watu hawajaitimiza, uliwawekea deadline, sitaongeza hata siku moja, na nitaomba unikabidhi hayo makaratasi, kila mmoja kule aliko lazima ajue, Wakurugenzi ambao wamekalia fedha za miradi sitaongeza siku hata moja.”

Aidha, Mchengerwa amesema watendaji ambao hawatimizi wajibu wao, wabadhilifu wa fedha za umma na wala rushwa hawatakuwa sehemu ya utendaji wake kwenye serikali hii.


Amesema pia hatakubaliana na uonevu wa watumishi na kuwataka maafisa utumishi katika mamlaka za serikali za mitaa kusikiliza kero za watumishi na kuzitatua.

“Kuwaonea watumishi hiyo sitakubali, kila mmoja sasa lazima aanze kujipanga, najua asilimia 76 ya watumishi wa umma wako TAMISEMI hivyo tunakazi kubwa ya kulinda haki za watumishi.”

“Nilipokuwa utumishi walinyooka, hivyo maafisa utumishi huko mliko nataka msikilize kero za watumishi kwenye maeneo yenu.”
Aidha, Mchengerwa ameweka bayana kuwa hayuko tayari kufanya kazi na mtumishi asiyefanyakazi na kusisitiza kuwa atamuweka kando.

“Katibu Mkuu (Adolf Ndunguru) utakuwa na kazi ya kufanya, yule asiyefanyakazi nitamuweka kando, sitakubali kwenda na mtu hataki kufanyakazi, sitakubali kwenda na afisa utumishi hasikilizi kero za watumishi, nilikuwa hakimu kwahiyo nilikuwa najua namna ya kugawa haki.”

“Ukifanya kazi na kutimiza majukumu yako kwa haki, utakiwa karibu na mimi, lakini ujanja ujanja na kufanyakazi kwa mazoea sio sehemu ya utendaji wangu wa kazi, kwa hiyo niwaombe lazima tubadilike.”

“Hufanyikazi nitakuweka kado nah ii ni kwa yoyote, hakuna gold father hapa kama mtu ameletwa na mtu kwa jina lazima afanyekazi kwa bidii na hii ni kwa kila mtumishi hii si kwa watendaji wa wizara pekee bali mpaka kijijini kama umepata kazi kwa jina la mtu ufanyekazi kwa bidhii sitakubali hata kidogo.”

Mchengerwa amesema Serikali imepeleka fedha nyingi za kutekeleza miradi katika mamlaka za serikali za mitaa na kubainisha kuna baadhi wasiotekeleza wajibu wao na kusisitiza kuwa hatamvumilia mtu yeyote.

“Serikali imepeleka fedha nyingi lakini miradi mingi haijamailika kwa watu kuiba, wanakula rushwa, ubadhilifu wa fedha miradi, uvivu na uzembe wengine wanafanya kampeni za siasa hawafanyikazi walizoteuliwa nazo, tutamshauri mheshimiwa Rais tutawaweka kando tunataka kila moja afanyekazi kwa bidhii ili tuweze kufanikiwa.”

Naye Waziri wa Malisili na Utalii, Angellah Kairuki alisema kwa kipindi cha miezi 10 aliyohudumu Ofisi ya Rais TAMISEMI kuna mambo yamefanyika na kufanikiwa huku ukusanyaji mapato kwenye halmashauri ambao umevuka lengo kwa zaidi ya asilimia 101.

Amesema pia wamehakikisha nidhamu ya utendaji kazi na uadilifu katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa inakuwa nzuri.

“Kwa sasa jukumu lililombele ni uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwakani na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo.”

“Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Malisili tutashirikiana sana, yako mambo mengi, ukiangalia kuna wanayamapori, maafisa misitu wako katika halmashauri. Kama kuna jambo liko kwa upande wetu tukutane na kuyazungumza badala ya kutumishiana misuli.”

Awali Naibu Waziri, Dk Festo Dugange alimhakikishia waziri kuwa watampa ushirikiano ili kufikia malengo ya nchi.
(mwisho)

No comments:

Post a Comment