PROF.NDALICHAKO AZITAKA TAASISI ZOTE KUHAKIKISHA WANA WATAALAMU WA LUGHA ZA ALAMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, September 20, 2023

PROF.NDALICHAKO AZITAKA TAASISI ZOTE KUHAKIKISHA WANA WATAALAMU WA LUGHA ZA ALAMA


Na Okuly Julius-Dodoma

Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ,(Kazi,Vijana,Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Prof.Joyce Ndalichako ,amezitaka taasisi za Serikali kuhakikisha wana Wataalamu wa Lugha za alama maeneo yao ya huduma ili kuhakikisha watu wote Wenye Ulemavu wanajumuishwa katika Fursa zote za maendeleo.


Prof. Ndalichako ameyasema hayo Leo Septemba 20,2023 wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya Wiki ya Kimataifa ya Viziwi Duniani yatakayofanyika kuanzia Septemba 25-30,2023 Jijini Mbeya.


"Malengo ya Serikali ni kuhakikisha Kila taasisi inakuwa na wataalam wa Lugha ya alama hivyo Miongozo imeandaliwa ni vyema kila taasisi ihakikishe watu wote Wenye Ulemavu wanajumuishwa katika Fursa zote za maendeleo,"amesema Prof.Ndalichako



Prof.Ndalichako amesema maadhimisho hayo yametokana na mahitaji na changamoto zilizokuwa zinawakabili Viziwi Duniani ndio maana ikatengewa wiki yake ambapo hufanyika Kila Mwaka wiki ya mwisho ya Mwezi Septemba.


"Serikali ya Tanzania inaungana na Viziwi wote Duniani katika maadhimisho ya Wiki hii na tunahimiza matumizi ya Lugha ya alama na ndio maana kauli Mbiu ya wiki hiyo Inasema "Dunia ambayo popote walipo Viziwi wanaweza kutumia Lugha ya alama"


Pia ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kuwathamini watu Wenye Ulemavu kwani wameshathibitisha kuwa Ulemavu wao sio kikwazo katika shughuli za maendeleo.


"nitoe rai kwa Wananchi wenzangu wa Tanzania kuwathamini na kuziunga mkono kazi zinazofanywa na Watu Wenye Ulemavu kwani wameshathibitisha kuwa sio kikwazo katika shughuli za maendeleo,"


Na kuongeza kuwa"ndio maana hata katika Serikali yetu hasa Awamu hii ya Sita Chini ya Dkt.Samia Suluhu Hassan amewapa nafasi za Uongozi watu Wenye Ulemavu katika Serikali yake na wanafanya vizuri sana hivyo tuwaamini na kuwathamini,"amesema Prof.Ndalichako.


Kwa upande wake  Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Viziwi Tanzania Adam Shabani Shaibu, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwezesha kuwepo kwa Wiki hiyo na kuwakaribisha Wananchi wote hasa wa Jiji la Mbeya kuhudhuria maadhimisho hayo kwani kutakuwa na Maonesho mbalimbali ya mambo yanayofanywa na Viziwi.


Ametoa wito Kwa Wananchi kujifunza Lugha ya Alama kwani changamoto hiyo inaweza kuwa Fursa kwao na kuifanya Lugha hiyo kuwa ya Mawasiliano ya kawaida.


No comments:

Post a Comment