Umeme kukuza shughuli za kiuchumi Msikisi - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, September 23, 2023

Umeme kukuza shughuli za kiuchumi Msikisi


Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali itahakikisha kila kijiji kinapata umeme ili wananchi wapate maendeleo.

Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Msikisi, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Naibu Waziri Kapinga
amesema, kufika kwa umeme katika kijiji cha Msikisi, kutakuwa ni chachu ya kukuza shughuli za kiuchumi Kijijini hapo.

Naibu Waziri Kapinga amesema shilingi Bilioni 6 zimeletwa katika Halmashauri hiyo ili kuweka umeme.

Aidha amesema, bado kuna vitongoji ambavyo havijapata umeme lakini baada ya kumalizika vijiji vitongoji navyo vitapata umeme ambapo katika Halmshauri hiyo shilingi Bilioni 7 zimetengwa kwa ajili ya kusambaza umeme katika vitongoji 79.

Ametoa wito kwa wakandarasi kufanya kazi kwa bidii ili vijiji walivyopangiwa kufikisha umeme wafanye hivyo ili azma ya Serikali ya kufikisha umeme kila kijiji ifanikiwe.

Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga ametoa wito kwa wananchi kutumia fursa hiyo kujiunganishia umeme katika nyumba zao.


No comments:

Post a Comment